Tuesday, 10 March 2020

DC TANO MWERA AHIMIZA WANAWAKE KUFANYA KAZI KWA BIDII KUEPUKANA NA UTEGEMEZI


NA MWANDISHI WETU

MKUU wa Wilaya ya Busega iliyopo Mkoa wa Simiyu, Bi. Tano Mwera  amewahimiza  wanawake nchini kote kufanya kazi kwa bidii kuepukana na utegemezi kwenye jamii zao.

Bi. Tano Mwera amesema hayo Machi 8, wakati wa kilele cha siku ya Wanawake Duniani ambapo amesema ndani ya Wilaya hiyo ya Busega Wanawake wanatakiwa kujituma kwenye shughuli mbalimbali za kijamii ikiwemo zile za kujipatia kipato sambamba na shughuli za kiuchumi.

"Kauli mbiu ya mwaka huu ni 'Kizazi cha Usawa kwa Maendeleo ya Tanzania  ya Sasa na baadae' Naendelea kuwahimiza Wanawake wote Busega na nchini kote tuthamini hutu wetu, tuendelee kufanya kazi kwa bidii kuepukana na utegemezi." Alieleza DC. Tano Mwera.

Mkuu huyo wa Wilaya ya Busega amekuwa mstari wa mbele katika kusaidia na kutetea Wanawake ambapo amefanya mambo mbalimbali  ikiwemo kuwezesha vikundi vya akina mama pamoja na mtoto wa kike ndani ya Wilaya hiyo.

Shughuli za siku ya Wanawake imefanyika Duniani kote huku kwa Tanzania kitaifa imefanyika Mkoani simiyu na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,  Samia Suluhu Hassan.

MWISHO.!

No comments:

Post a Comment