Katibu Tawala wa wilaya ya Arusha David Mwakiposa akiongea kwenye hafla ya makabidhiano ya vifaa kwa wamiliki wa magari ya Unyonyaji wa Maji Taka kwenye ukumbi wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Arusha picha zote na Ahmed Mahmoud Arusha

Katibu Tawala Jiji la Arusha David Mwakiposa akimkabidhi vifaa vya kufanyiakazi ya Unyonyaji wa Maji Taka kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Sifael Silanga kwenye makabidhiano yaliofanyika kwa ukumbi wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Arusha

Na Ahmed Mahmoud Arusha
Katibu Tawala wa wilaya Arusha David Mwakiposa amewataka wananchi wa Jiji la Arusha kuhakikisha wanayaweka katika hali ya Usafi  wa mazingira ya maeneo yao ili kuweza kuepukana na milipuko ya Magonjwa.  

Aliyasema hayo kwenye hafla ya makabidhiano ya vifaa Kinga kwa wamiliki wa makampuni yanayofanya usafi wa mazingira Jiji la Arusha vilivyotolewa na shirika la Maendeleo la Uholanzi iliyofanyika kwenye ukumbi wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Arusha jijini hapa.

Alisema kuwa ,ili wananchi wa Jiji la Arusha waweze kuishi maisha mazuri yenye usalama na Afya nzuri ni jukumu lao kuhakikisha wanayaweka mazingira yao katika hali ya Usafi kila wakati kwa lengo la kuepukana na milipuko ya Magonjwa.

Akaitaka halmashauri ya Jiji la Arusha kuhakikisha wanasimamia vifaa walivyopewa na wafadhili na vinatumika kwa mahitaji yaliopangwa huku wakihakikisha wanatoa taarifa kila mwezi za  waharibifu wa  mazingira na hatua zilizochukuliwa.

Awali akimkaribisha mgeni rasmi Mratibu wa kampeni ya  taifa ya Usafi wa mazingira Jiji la Arusha ,Allan Rushokana alisema vifaa kinga hivyo vina thamani ya milion 4.8 na vinatolewa kwa kampuni 7 zinazofanyakazi ya Unyonyaji wa maji taka ndani ya Jiji hilo.

Akatoa wito kwa wananchi kuendelea kutumia huduma hizo kwa lengo la kuhakikisha wanayaweka mazingira yao katika hali ya Usafi itakayosaidia kuondokana na maradhi ya milipuko ambayo yanaweza kuepukika wakitumia huduma za Unyonyaji wa maji taka kwa wakati.

Alisema kuwa Jiji hilo kupitia mradi huo watahakikisha linakuwa kwenye hali ya Usafi wa mazingira na watakuwa wakali pindi watakapoona sheria za mazingira zikivunjwa na kuwataka wananchi kufuata sheria na kuyaweka mazingira katika hali ya Usafi kwa maisha Bora ya kila siku.

Nae Mshauri wa Mradi wa Maji na usafi wa Mazingira Sauli  kutoka shirika la Maendeleo ya Uholanzi (SNV),Sauli Mwandosya alieleza kuwa baada ya kufanya utafiti wa kina waligundua kuna changamoto kubwa ya watu kufanya kazi za Usafi wa mazingira bila vifaa ndio maana wakaanzisha utoaji wa elimu na vifaa kwa makampuni ya Usafi wa mazingira Jiji la Arusha kwa lengo la kuondoa changamoto na kuepuka magonjwa.

Naye Mratibu wa programu wa elimu ya Afya mashuleni Jiji la Arusha,Monica Ngonyani alisema kuwa,mradi wa usafi wa mazingira mjini ni mradi unaotekelezwa na halmashauri ya Jiji la Arusha kwa kushirikiana na mamlaka  ya maji safi na Usafi wa Mazingira (AUWSA)ambapo mradi una huu umejikita katika kuboresha mnyonyoro wa huduma ya usafi wa Mazingira hususani uthibiti wa kinyesi Cha binadamu.

"mradi huu ni wa miaka mitano ulioanza 2017 hadi 2022 na wafadhili wakuu ni kitengo maalumu ndani ya wizara ya mambo ya nje ya Uholanzi,ambapo walengwa wakuu wa kufikiwa na mradi ni kaya,shule,vituo vya kutolea huduma tiba,watoa huduma ya Unyonyaji wa tooe kinyesi ,na vyoo vya umma'alisema Monica.
Share To:

Arusha Newsroom

Post A Comment: