Saturday, 22 February 2020

JITIHADA ZA ARIF ABRI ZAPONGEZWA IRINGAMjumbe wa mkutano mkuu wa CCM Taifa  Arif Abri akiwa viongozi wa jumuiya za CCM wilaya ya Iringa vijijini 

JUMUIYA  ya  wazazi wa chama  cha mapinduzi  (CCM)  wilaya ya  Iringa  vijijni mkoani Iringa  imepongeza  jitihada mbali mbali  zinazofanywa na mjumbe wa  mkutano  mkuu wa CCM Taifa  anayewakilisha  wilaya ya  Iringa vijijini Arif Abri katika  kuiwezesha  jumuiya  hiyo  kuwa na miradi yake.

Mwenyekiti  wa  jumuiya  hiyo Marco Kihongo alisema kuwa pamoja na misaada mbali mbali anayotoa maeneo mengine ndani ya jama na jamii pia Abri amekuwa hachagui kusaidia .

Alisema kwa upande wa jumuiya hiyo pamoja na misaada mingine amepata kuchangia   pesa  kiasi cha shilingi milioni 1  kwa ajili ya kutekeleza  ahadi yake aliyoitoa kwa jumuiya  hiyo   ya  kuchangia  pesa hizo kwa ajili ya  ununuzi wa kadi  za jumuiya kwa  wanachama  wapya.

Kihongo alisema  kuwa mchango huo  wa  fedha  ni mtaji mkubwa kwa  jumuiya  hiyo kuweza kuongeza idadi kubwa  zaidi ya  wanachama wake  na  kuwa zoezi la  uongezaji  wanachama  litaanza mara moja  kuanzia sasa .Katibu wa mbunge wa jimbo la Ismani ,Wiliam Lukuvi alisema  kuwa  jitihada kubwa  zimekuwa  zikifanywa na  Arif Abri katika  wilaya ya  Iringa  ni mfano wa kuigwa na  kuwa kazi mbali mbali amekuwa  akichangia  hivyo  kuchangia fedha  hiyo ni mwendelezo wa misaada mbali mbali ambayo amekuwa akitoa.

"  Tunaamini Mungu  humjalia   zaidi  yule anayetoa kwa  ajili ya  wengine  kifupi  tunashukuru  sana  kwa  misaada  mbali mbali ya kijamii na  chama katika  wilaya  ya Iringa vijijini "  alisema Thom 

Arif alisema wajibu wake ni kujenga chama na kuunga mkono jitihada za serikali ya awamu ya tano chini ya CCM na ataendelea kufanya hivyo .


" nimeendelea kusaidia jumuiya zote na hivi  karibuni   wakati namtafuta  katibu wa jumuiya ya  wazazi  nilimpigia  mwenyekiti wa  umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi (UVCCM)wilaya ya Iringa vijijini ambae pia  aliomba kusaidia  pikipiki  nilimuahidi kuwa asiwe na hofu  nitampa  pikipiki   hiyo na nimewakabidhi tayari  "  alisema Arif 

No comments:

Post a comment