NA HERI SHAABAN
HOSPITAL ya Rugambwa iliyopo wilayani Ilala wajivunia mafanikio kwa kutoa huduma bora na kuongeza jengo jipya la matibabu ya figo .

Akizungumza mafanikio hayo Leo wakati wa uzinduzi wa jengo hilo Mganga Mkuu wa hospital hiyo Dkt. Sarah Deogratius alisema kwa ushirikiano wa Africa Health care Network (AHN) wamefanikisha ujenzi wa jengo la     matibabu ya figo ili kusogeza huduma bora kwa wananchi.

"huduma hii ya matibabu ya  figo   ni muhimu na umekuwa na uhitaji mkubwa kwa wagonjwa wetu hukizingatia eneo hili halina huduma hii hivyo kuanzisha kwa huduma hii kutarahishisha kupunguza gharama za nauli kufuata matibabu mbali" alisema Dkt. Sarah

Dkt. Sarah alisema wamejitahidi kufuata miongozo wizara ya Afya na Ustawi na Jamii  ili huduma hiyo iweze kuwa bora ya magonjwa ya figo na kuwafaa wananchi watakaotumia.

Alisema mpaka kufikia mafanikio hayo wamepata ushirikiano ofisi ya Mganga Mkuu halmashsuri ya Ilala na Mkoa Dar es salaam.

Aidha alisema halmashauri ya Ilala  itaiwezesha hospitali hiyo hilingi milioni 100 ambazo wamesaini hivi Karibu fedha za mfuko wa afya (Busket fund)  kwa ajili ya huduma ya mama na mtoto.


Alisema kujifungua kawaida ilikuwa  100,000/= sasa ni shilingi 50,000/= upasuaji shilingi 400,000/= kwa sasa shilingi 200,000/= ili kuwasaidia wananchi wa kipato cha chini  hasa wanawake Wajawazito na watoto wenye miaka 5 kupata gharama nafuu katika hospitali hiyo.

Mafanikio mengine   Wanafunzi kujifunza na kuongeza ujuzi mfano vyuo vya Kampala (KIU)  Masada, Hurbert, Kairuki, Ruaha, University College, (Ruco) Iringa, City Colledge, na Paradize.

Kwa upande wake Kaimu Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Ilala Dkt. Wile Sangu alisema hospitali ya Cardinal Rugambwa ni kituo muhimu inaisaidia halmashauri ya Ilala katika kuwahudumia wagonjwa wa pembezoni ambao wanashindwa kufika katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa Amana.

Dkt, Sangu  alisema Manispaa ya Ilala inashitikiana na kituo hicho pia Serikali imekisaidia kituo hicho fedha milioni 100 zimeelekezwa katika huduma ya mama na Mtoto.

Naye Mgeni rasmi Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Dkt. Yudas Ndungulile aliwapongeza kwa ufunguzi wa jengo hilo ili kutoa huduma kwa wagonjwa wa figo.


Amewataka wafanye kazi kwa weledi katika kuwahudumia wateja ili wapate huduma nzuri za afya  .

Katika hatua nyingine aliwataka watumishi wa hospitali hiyo kutunza vifaa vya matibabu.

Mwisho
Share To:

msumbanews

Post A Comment: