Tuesday, 21 January 2020

WATENDAJI WA KATA NA VIJIJI MBEYA WAONYWA


Kuna stori nimetuma kwa email hao ni watendaji wa Kata wakipokea bati zilizotolewa na mfuko wa Jimbo

Na Esther Macha,Mbeya

KAIMU ofisa mipango wa halmashauri ya Wilaya ya Mbeya,Oscar Matingo  amewataka watendaji wa kata na vijiji waliopokea  vifaa kutokas mfuko wa jimbo kutoweka maofisini badala yake vifanye kazi iliyokusudiwa ili kutowavunja moyo wananchi ambao wanaibua miradi ya maendeleo.

Matingo aliyasema hayo jana  kwenye ofisi za halmshauri ya wilaya ya Mbeya wakati wa kukabidhi  vifaa hivyo kwa watendaji hao ambavyo vimetolewa na mfuko wa jimbo ili kusaidia miradi ya wananchi waliyoibua vijijini  na kuanza kuitekeleza kwa nguvu zao wenyewe.

Kwa upande wake Ofisa mtendaji wa Kijiji cha Ihombe  wilaya ya Mbeya ,Mariam Sokolo alisema kuwa  mfuko wa jimbo umekuwa ukisaidia kupiga hatua za ujenzi kwani kijiji chetu tumepokea bati za zahanati .

Alisema katika ujenzi huo wa zahanati ilikuwa bati hivyo wamefurahi kupata bati hizo ambapo zitaweza kusaidia kuezeka zahanati hiyo.

Naye katibu wa Mbunge wa  Jimbo la Mbeya vijijini ,Essau Janga alisema kwamba toka wanaanza wananchi wamekuwa wakifanya vizuri kwa kutoa ushirikiano kwa mfuko wa jimbo katika kuibua miradi ya maendeleo.

Alisema vifaa vilivyotolewa ni mifuko ya saruji mifuko ya saruji 1930,Bati 660, pamoja na kugawa fedha mil.11.1 pamoja na mil.5.4 kwa ajili ya shughuli za ufuatiliaji.


No comments:

Post a comment