Mbunge wa Jimbo la Songea Mjini kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi(CCM)Dkt,Damas Ndumbaro amewataka wakazi wa jimbo hilo kuendelea kumuunga mkono pamoja na Serikali iliopo madarakani ili izidi kuwaletea maendeleo.mwandishi Amon Mtega anaripoti kutoka Songea 

Wito huo aliutoa  wakati akiwahutubia wakazi wa kata ya Mshangano Manispaa ya Songea mkoani humo kwenye mkutano wa hadhara ambao ulihudhuliwa na wakazi wengi wa kata hiyo pamoja na kupata nafasi ya kuwasilisha baadhi ya changamoto zilizopo kwenye kata hiyo.

 Mbunge Dkt ,Ndumbaro ambaye pia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki amesema kuwa Serikali ya awamu ya tano inayo ongozwa na Rais Dkt John Pombe Magufuli  imekuwa ikiendelea kuwaletea maendeleo Wananchi wake ,hivyo ni vema Wananchi wakaendelea kuiunga mkono kwa kuipatia ridhaa tena.

 Dkt,Ndumbaro akijibu baadhi ya changamoto za Wananchi wa kata hiyo ikiwemo suala la Maji ya bomba kukosekana kwa baadhi ya mitaa amesema kuwa tayari fedha zimeshapatikana za kuongeza chanzo kingine cha Maji ambacho kipo Mahilo Nje kidogo ya Manispaa hiyo ambacho watalaamu wameshakifanyia utafiti kuwa kitaweza kusambaza Maji mji mzima kwa kila kaya.

 Amefafanua kuwa kwa upande wa Umeme Serikali imeshajipanga ifikapo mwaka 2021 kila kijiji na kila kaya watakuwa tayari wameingiziwa Umeme ,katika suala la Barabara za Mitaa ikiwemo barabara ya Namanyigu inayounganisha na kata ya Mletele ambayo ni moja ya Barabara mhimu ambayo Barabara kuu ikifunga magari yaendayo mikoa mingine hutumia hiyo,ambayo nayo amesema ataifanyia kazi kwa kuwashirikisha Wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini(Tarura).

 Aidha ombi la kutaka Wananchi wazungushe Vibanda vya Biashara katika eneo la Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC)ni wazo nzuri bali mchakato huo uanzie kwenye vikao husika vikiwemo vya Serikali za mitaa (WDC) ambavyo vitasaidia ombi hilo kwa wahusika wa eneo hilo .

 Kwa upande wake mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM)Wilaya ya Songea Mjini ,Hamis Abdal Ali amewataka Viongozi waliochaguliwa katika Serikali za mitaa kuacha malumbano na badala yake wafanye kazi za Wananchi ambao wamewatuma.
     
Share To:

Francis Godwin Mzee wa matukiodaima

Post A Comment: