Waziri wa Sera,Bunge,Kazi,Vijana,Ajira na Walemevu Mhe. Jenista Mhagama akitoa maelekezo leo .
......................

Na.WAMJW-Mwanza

IMEELEZWA kuwa sasa watanzania milioni.1.4 wanaoishi na VVU ambapo kiwango cha maambukizi.kimesimama kwenye.asilimia 4.7 ikilinganisha na asilimia 7.0 ya mwaka 2014.

Hayo yamesemwa leo na Mgeni rasmi wa maadhimisho ya kitaifa ya siku ya UKIMWI duniani  na Waziri wa Sera,Bunge,Kazi,Vijana,Ajira na Walemevu Mhe. Jenista Mhagama jijini hapa.

Waziri Mhagama amesema kuwa maambukizi mapya na vifo  vitokanavyo na UKIMWI pia vimepungua.

"Tumeweza kupata mafanikio haya kufuatia kuboreshwa kwa huduma.za ART na afua za kinga kama vile utahiri wa kitabibu wa wanaume na kuzuia maambukizi ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto"Alisema Waziri Mhagama.

Aidha, amesema kiwango  cha watu wanaoishi na VVU walioko kwenye mpango wa ARV kimeongezeka kutoka asilimia 22 mwaka 2009 hadi kufikia asilimia 57 ya mwaka 2017.

Naye Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amesema mpaka kufikia mwezi Septemba 2019 takribani watu 1,252,205 kati ya wananchi 1,600,000 wanaokadiriwa kuishi na VVU nchini walikuwa wamepima na kufahamu hali zao za maambukizi ya VVU.

"Hii ni sawa na asilimia 78.3 ya lengo la 90 ya kwanza.
Miongoni mwao wanaume walikuwa 413,985 sawa na asilimia 33, na wanawake walikuwa 838,220 sawa na asilimia 77".

Kwa upande wa vijana Waziri Ummy amesema kuwa Vijana balehe (umri wa miaka 10 – 19) walikuwa 57,167 sawa na asilimia 4.6, na vijana (umri wa miaka 15 – 24) walikuwa 96,006 sawa na asilimia 7.7.

Aidha, amesema kati ya waliopima na kutambua afya zao watu 1,221,799 sawa na asilimia 97.6 wanatumia ARV.

Hata hivyo alisema Lengo la 90 ya pili ambalo ni asilimia ya kuwa watu waliopimwa na kugundulika kuwa wana maambukizi ya VVU wanatumia dawa za kupunguza makali ya VVU (yaani ARV’s), tayari tumefikia takriban asilimia 98 wanatumia zawa za kupunguza makali ya VVU yaani ARV.

"Lengo la 90 ya tatu, ambalo ni kuhakikisha kuwa asilimia 90 ya wanaotumia ARV’s wamefanikiwa kupunguza wingi wa VVU mwilini Waziri huyo alisema wamefanya vizuri sana,"ni kuwa tumekuwa tukifuatilia kwa karibu hali za watu wanaotumia dawa za kupunguza makali ya VVU".Alisema

Waziri Ummy alitaja mafanikio mengine ya kujikinga dhidi ya maambukizi ni tohara kwa wanaume ambapo kuanzia mwaka 2009 hadi Agosti 2019 jumla ya wanaume 4,456,511 wamefanyiwa tohara kupitia njia za mkoba na huduma katika vituo vya huduma

Takwimu zinaonesha kwamba watu 953,973 sawa na asilimia 89 ya watu 1,072,650 waliopimwa wingi wa VVU wamefanikiwa kupunguza wingi wa VVU mwilini jambo ambalo ni muhimu katika kinga dhidi ya UKIMWI.Kauli mbiu ya maadhimisho ya mwaka huu ni "Jamii ni chachu ya mabadiliko,tuungane kupunguza maambukizi mapya ya VVU"
Share To:

Francis Godwin Mzee wa matukiodaima

Post A Comment: