.Wataalamu wa NHIF mkoa wa Pwani wakihamasisha waumini wa kanisa Katoliki la Tumbi Kibaha kujiunga na vifurushi vya bima ya afya.
Baraka Massawe (pichani) kulia akitoa elimu na kuwahamasisha waumini wa kanisa Katoliki la Tumbi Kibaha kujiunga na vifurushi vipya vya bima ya afya

.....................................................
WATAALAMU wa mfuko wa Taifa wa Bima ya afya (NHIF) mkoa wa Pwani wamepiga kambi katika kanisa Katoliki la Tumbi lililopo mjini Kibaha kwa ajili ya kutoa elimu na kuhamasisha waumini wa kanisa hilo kujiunga na vifurushi vya bima ya afya. Mwandishi Gustaphu Haule anaripoti toka Pwani .

Kambi hiyo imefanyika jana Jumapili ikiwa ni muendelezo wa kampeni ya kutoa elimu na kuhamasisha wananchi kujiunga na vifurushi vipya vya bima ya afya vilivyotangazwa hivi karibuni na Serikali kupitia Wizara ya Afya.

Miongoni mwa wataalamu hao ni Yusta Makulusa ,Baraka Massawe na Hadija Litami timu ambayo ipo chini ya meneja wa Nhif Mkoa wa Pwani Ellentruda Mbogoro.

Akizungumza katika kampeni hiyo Mbogoro ,alisema kuwa Nhif inaendelea na mpango wa kutoa elimu katika maeneo mbalimbali ikiwemo kanisani na misikitini na kwamba lengo ni kuwafikia wananchi wengi zaidi.

Mbogoro,alisema Nhif inaamini kuwa maeneo ya kanisani na misikitini kuna idadi kubwa ya watu na kwamba lazima waumini wake wafikiwe kwa ukaribu ili wapate elimu ya kutosha.

"lengo la Nhif ni kuhakikisha kila waumini wa makanisani na misikitini wanafikiwa na elimu hii ya vifurushi vipya ili kila mtu haweze kujiunga kwa ajili ya kupata matibabu kirahisi",alisema Mbogoro

Mbogoro,alisema kuwa vifurushi hivyo ni Najali Afya,Timiza Afya na Wekeza Afya na kwamba kila mtu anaweza kujiunga kulingana na umri wake na uwezo wake wa kipato.

Mbogoro aliwataka Wananchi na jamii kiujumla kujiunga na huduma hizo kwakuwa ni fursa ya kupata matibabu kirahisi pale wanapougua.

Baadhi ya waumini wa kanisa hilo akiwepo Richard Michael,alisema kuwa fursa hiyo ni nzuri kwa wananchi lakini aliiomba Serikali kuangalia upya namna ya kuboresha gharama zilizowekwa kwenye vifurushi hivyo.

Nae Odila Kihaule,alisema kuwa kuna haja ya Nhif kuwafikia wananchi waliopo Vijijini kwakuwa wengi wao wanakosa elimu hiyo na hivyo kukosa fursa ya matibabu ya bima ya afya pale wanapougua.

MWISHO.
Share To:

Francis Godwin Mzee wa matukiodaima

Post A Comment: