<
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kilolo Aloyce Kwezi wakifurahia baada ya wilaya ya Kilolo kupewa tuzo ya elimu 
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Hamid Njovu akiwa ameshika kombe baada ya kupongezwa na mkoa kwa Manispaa hiyo kushika nafasi ya kwanza kwa ufaulu wa wanafunzi darasa la saba mwaka 2019 na nafasi ya nane kitaifa 
Mzee David Butinini kushoto akimpongeza mkuu wa wilaya ya Mufindi Jamhuri Wiliam kwa kutatua changamoto za elimu Mufindi  
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mufindi Netho Ndilito 

Mkuu wa mkoa wa Iringa Ally Hapi (wa nne kulia waliokaa)akiwa na viongozi mbali mbali na watendaji wa Kilolo 
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Mafinga Saada Mwaruka na mkurugenzi wa Kilolo Aloyce Kwezi wakifurahia zawadi ya kombe kwa kufanya vizuri katika elimu 
Wadau wa elimu mkoa wa Iringa wakiwa katika kikao cha elimu 
Mkuu wa mkoa wa Iringa Ally  Hapi amekutana na wadau wa elimu kuweka mkakati wa kuhakikisha wanafunzi wote waliofaulu kwenda sekondari wanaanza masomo yao ya sekondari mwakani 2020 .Mwandishi Francis Godwin anaripoti kutoka Iringa

Hapi amekutana na wadau hao wa elimu pamoja na viongozi wote wa Halmashauri za mkoa wa Iringa na kuweka mkakati  kukabiliana na changamoto ya upungufu wa madawati pamoja na nyumba vya madarasa inafanyiwa kazi mapema.

Mbali ya kuweka mkakati huo wa kukabiliana na changamoto ya madawati na nyumba vya madarasa amewataka viongozi wa wilaya ambazo zinachangamoto ya nyumba vya madarasa na madawati kutokwenda likizo wala kutoka nje ya wilaya zao  ili kusimamia utekelezaji wa ujenzi wa nyumba vya madarasa na madawati

Pia Hapi amepongeza  Halmashauri ya Manispaa ya Iringa chini ya mkurugenzi wake Hamid Njovu viongozi wote na mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela kwa kushika nafasi ya kwanza kimkoa kwa ufaulu wa wanafunzi mtihani wa Taifa wa darasa la saba mwaka 219 na kushika nafasi ya nane kitaifa 

Huku akipongeza  wilaya ya Mufindi kwa kufanya vizuri katika ujenzi wa nyumba vya madarasa na utengenezaji wa madawati ya kutosha kiasi cha kujihakikishia watoto wote waliofaulu kwenda sekondari wanaanza masomo yao kwa wakati mwakani 2020.

Hapi alieleza kushangazwa na wilaya za mkoa wa Iringa zinye upungufu wa madawati wakati mkoa wa Iringa unaongoza kwa kuwa na miti mingi ya kupata mbao na kutaka kuweka mkakati wa kutumia miti hiyo kumaliza changamoto ya madawati  kama walivyofanya wilaya ya Mufindi .

Alisema Halmashauri ya Mji Mafinga chini ya mkurugenzi Saada Mwaruka imeonyesha kuwa na mkakati mzuri wa kuwaandaa wanafunzi wake na ufaulu na jinsi ya kutatua changamoto za elimu na kuzitaka Halmashauri nyingine kumtumia afisa elimu wa Halmashauri hiyo kujifunza mkakati hiyo huku akimwagiza Afisa elimu mkoa kutenga bajeti na  siku ya maofisa elimu kukaa pamoja ili afisa elimu wa Mji wa Mafinga kujifunza na yeye atampatia kiasi cha shilingi 500,000  afisa elimu huyo kama pongezi kwake .

Pia aliipongeza Halmashauri ya Mufindi chini ya mkurugenzi wake Netho Ndilito kwa kuhakikisha wanafunzi wote zaidi ya 3505 waliofaulu mtihani wa darasa la Saba mwaka huu wanaanza masomo yao mwakani sekondari .


Pamoja na Halmashauri hizo mkuu wa mkoa amepongeza Halmashauri ya Kilolo chini ya mkurugenzi wake Aloyce Kwezi na viongozi wote wa wilaya ya Kilolo chini ya mkuu wa wilaya Asia Abdallah kwa kufanya jitihada ya kupanda kiasilimia katika ufaulu wa wanafunzi na kuwazawadia zawadi ya kombe .


Aidha mkuu wa mkoa kupitia kikao hicho amewapongeza wanafunzi, walimu na wilaya zilizofanya vizuri katika matokeo ya mtihani wa Taifa wa darasa la Saba kwa kuwapa zawadi mbalimbali.


Share To:

Francis Godwin Mzee wa matukiodaima

Post A Comment: