Mwenyekiti mpya wa Miomboni katika Halmashauri ya Mji wa Babati Mathias Zebedayo ameahidi kufanya mambo makubwa ya kimaendeleo MWANDISHI JOHN WALTER ANARIPOTI TOKA BABATI
Mwenyekiti huyo ni miongoni mwa wenyeviti wa chama Cha Mapinduzi (CCM) waliopita bila Kupingwa katika uchaguzi wa serikali za mitaa uliofanyika Novemba 24,mwaka huu.
Zebedayo ameahidi kushughulikia kero mbalimbali zinazowakabili wananchi wake ikiwa ni pamoja na upatikanaji wa huduma ya umeme, Miundo mbinu ya Bara bara inayounganisha mitaa mbalimbali na kuwaweka wananchi pamoja bila kujali tofauti za itikadi za vyama kwa kuwa lengo ni kuleta maendeleo.
Kwa kipindi cha uongozi wake katika mtaa huo muhula uliopita, amemueleza mwandishi wa habari hizi kuwa amefanikiwa kurudisha eneo la shule ya msingi Miomboni lililokuwa limevamiwa na watu kinyemela,kwa kumwandikia barua waziri wa ardhi, nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi.
Mwenyekiti huyo amesema ujenzi wa shule ya msingi Miomboni utaanza muda wowote kwa nguvu za wananchi ili kuwaondolea adha watoto kwenda umbali mrefu kufuata shule.
Post A Comment: