Makamu mwenyekiti wa CCM Tanzania bara Philip Mangula kulia akimkabidhi katibu mkuu wa CCM Taifa Dkt Bashiru Ally hati ya shukrani kwa  mchango wake katika chuo cha vijana Ihemi 

Viongozi mbali mbali wakiwa katika ufunguzi wa chuo cha vijana Ihemi 


Katibu mkuu wa CCM Taifa Dkt Bashiru Ally katikati na MNEC Taifa Salim Abri Asas kulia wakimhoji binti fundi kushona chuo cha vijana Ihemi 

.......


KATIBU   mkuu  wa chama  cha mapinduzi ( CCM) Taifa Dkt  Bashiru  Ally ameutenga rasmi  uongozi wa  umoja  wa  vijana  wa chama cha mapinduzi (UVCCM)  katika bodi ya  vyuo  vya UVCCM baada ya   kuteua bodi ya muda ya  watu 9  itakayosimamia  chuo  hicho ikiongozwa na mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa     huku mjumbe  wa Halmashauri kuu ya  CCM Taifa anayetoka  mkoa wa Iringa Salim Asas  akiingizwa kuunda bodi hiyo .

Akitangaza  bodi  hiyo   itakayosimamia  chuo   hicho jana  baada ya  uzinduzi wa chuo hicho ulioongozwa na makamu  mwenyekiti wa CCM Taifa  Philip Mangula alisema  kuwa lazima CCm kujenga  wanachama  wenye  moyo wa kukuza  moyo wa   kujitolea  kwani  alisema   chuo  hicho hadi sasa  kimejengwa kwa kiasi cha  zaidi ya shilingi milioni 800  na kuna  watu  ambao  walijitolea kwa kulala katika ujenzi wa chuo hicho na kushiriki shughuli mbali mbali  kwa  kujitolea  na bila  wao  chuo hicho kisingekuwepo .

"  Ili  kuanza  kusimamia  vizuri na kwa sababu hakujawa na utaratibu  ambao umepitishwa  kamati kuu wa kuendesha  vyuo hivyo ambavyo vinafufuliwa  chuo   cha Ihemi na  vingine  natangaza bodi ya muda   ya  kushauri namna ya kuendesha na kusimamia vyuo  hivyo  wakati utaratibu wa kamati kuu  unaandaliwa natangaza   vyeo  vya  watakaosimamia  bodi  hiyo  si kwa majina  "  alisema  Dkt Bashiru 

Kuwa  atakayekuwa   mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa atakuwa  mwenyekiti wa  bodi ya ushauri ,atasaidiwa na atakayekuwa  mkuu wa   chuo ndie  atakuwa katibu  wa  bodi hiyo na  kwa kuwa bado hajateuliwa basi  katibu wa CCM mkoa wa Iringa atakaimu  nafasi hiyo  hadi pale  nafasi  hiyo  itakapojazwa .

wajumbe  wengine ni mlezi wa CCM mkoa wa Iringa  waziri mkuu mstaafu Mizengo Pinda  yeye  atawakilisha kamati kuu katika  bodi hiyo  na anaanza mara  moja ,mjumbe  mwingine ni  MNEC wa Iringa hata akiondoka  yeye  mwanachama  atakayekuwa MNEC wa  Iringa ndio atakayeshika nafasi hiyo , makatibu wa jumuiya za  CCM mkoa  na katika   hilo watachaguliwa  watu kwa  uwezo  na kama  hawatatosha  kwa sifa basi wataletwa watakaotosha .

Pia  mlezi wa jumuiya ya  vijana  Taifa ,idara ya itikadi na  uenezi itaweka pia  mjumbe  wake  wakati makao makuu ya umoja  wa vijana  itafanya kazi ya  kuratibu ,kuweka  mikakati na kupitisha na malengo makuu  kwa sababu  wao  pia  wana  vyuo vingine  .

"  Tunataka mkoa  wa Iringa ushiriki  vizuri na uongozi wake  kutusaidia kuendesha   chuo  hiki na wote  hao watakuwa chini ya  ofisi  yangu mimi katibu mkuu  bodi hii  itaanza kazi kuanzia  leo hadi hapo  kamati kuu itakapoweka  bodi ya  kudumu "


Dkt Bashiru alisema ili kuanza kusimamia vizuri vyuo vya UVCCM ambavyo vinafufuliwa kama Ihemi na Kibaha bodi hiyo itasaidia kuwashauri vijana wanaopata mafunzo katika vyuo hivyo na kuwasaidia kuacha kufikilia kuajiriwa.


“Natangaza bodi ya muda ya kushauri namna ya kuendesha vyuo hivyo wakati utaratibu wa kamati kuu unaandaliwa bodi hiyo itaundwa na watu wafuatao kwa vyeo sio majina, Mwenyekiti wa mkoa wa Iringa ambaye atakuwa ndio mwenyekiti wa bodi ya vyuo hivyo,atasaidiwa na atakayekuwa mkuu wa chuo na atashika nafasi ya katibu wa bodi,wajumbe wengine ni mlezi wa chama atawakilisha kamati kuu ya bodi hiyo”.

Awali akizindua majengo na miradi ya maendeleo ya chuo cha mafunzo Ihemi Makamu Mwenyekiti wa CCM Philip Mangula aliwataka vijana kufuta fikra za kufikiria kuajiliwa badala yake wafikirie kujiajiri.

“mnapokuja kwenye mafunzo hapa chuoni nataka mfute kabisa mawazo ya tunajifunza ili tukaajiriwe,hapa sehemu ya mafunzo ni kubadilisha fikra na mitizamo ya kwamba kusoma ni kuajiriwa”alisema

Mangula alisema kuwa vijana wabadili mitizamo ya kusoma ni kuajiriwa wengi wasome wakijua watajitegemea na chuoni hapo watafundishwa namna ya kujiajiri kwani ajira kubwa ni kilimo.

Kwa upande wake Mlezi wa CCM Mkoa wa Iringa Mizengo Pinda alisema moja ya malengo ya chuo hicho ni kujenga hisia  ndani ya vijana juu ya siasa ya nchi hii kwa maslah ya watanzania.

Alisema ni muhimu vijana kutambua uzalendo ni kitu gani hivyo unapoanza mafunzo ni muhimu kujikita katika siasa na itikadi ili waweze kujua taifa linataka nini kwa upande wa chama.

“Nimependezwa kuona chuo cha mafunzo ihemi kimekuwa ni kituo cha kuamsha hali na fikra mpya kwa vijana kisiasa na kimaendeleo,mna hekali 1963 yatatumika katika majengo lakini vilevile zitatumika katika kutoa mafunzo katika uzalishaji,kuna vitalu nyumba ufugaji wa nyuki na kilimo kwa ujumla”alisema

Naibu Waziri,Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi ajira na Vijana Antony Mavunde alisema vijana zaidi ya 200 katika chuo hicho walifundishwa kilimo kupitia kitalu nyumba na vijana 60,walifundishwa kupinda vyuma na kupitisha neti.

“Lengo lilikuwa ni baada ya muda mfupi tuwe na uwezo wa kuwatoa vijana wengi zaidi kutengeneza green house badala ya kuagiza nje ya nchi kama ilivyo sasa”alisema Mavunde

Waziri  wa Ardhi  ,nyumba na maendeleo ya makazi Wilima Lukuvi alisema kuwa  chuo  hicho  kimetengenezwa  vizuri na wanahakika chuo  hicho kiktakuwa mkombozi na kumshukuru Rais Dkt John Magufuli kwa kutoa kibali cha kuanzisha  chuo  hicho ambacho ni msaada mkubwa kwa vijana kwani kilipoanza kilikuwa na malengo kama hayo ila hayakutimia .

Mkuu wa Mkoa wa Iringa Ally Hapi alisema wakati wa ukombozi kazi kubwa ya chama ni hamasa,lakini baada ya uhuru siasa imebadilika imekuwa sayansi ni wakati sasa vijana wapate kufundishwa namana ya kujenga hoja na kupigania chama na kukilinda.

Christpher Ole sendeka Mkuu wa mkoa wa Njombe alisema anaipongeza CCM kwa kuyafufua mawazo ya Mhasisi wa taifa Julius Nyerere Kwa vitendo kwa kukifufua chuo hicho cha CCM.

“Huwezi kuwa na chama mazubuti chama makini bila kuwa na mahali pa kuwapika viongozi wake,chuo cha Ihemi kitaipa CCm nguvu mpya itakayoendana na kasi ya Rais wa Jamuhuli wa Tanzania Rais  John Magufuli”alisema

Chuo cha Ihemi ni chuo cha kihistoria ambapo kwa muda mrefu kilisimama kutokana na changamoto mbalimbali,ambapo leo kimefufuliwa upya na kitakuwa na miradi 21 ambapo mpaka kukamilika kwake kitagharimu kiasi cha 24 bilion na kinatarajia kutoa ajira kwa zaidi ya vijana 14000.


Kabla ya  katibu  mkuu kutangaza  rasmi uamuzi  wake  huo aliyekuwa kaimu katibu  mkuu wa UVCCM Taifa Shaka Shaka  alisema yeye  ndie  alifanya kazi kubwa ya  kupambania   chuo   hicho  hadi  leo kimeanzishwa  hivyo hata kama  hayupo katika  uongozi wa  vijana kazi aliyeifanya  ni kubwa .

"  Wakati  wa  wa  uongozi  wangu nilipotembelea  Ihemi  na kukuta  hali mbaya ya  chuo wa kwanza kumpigia simu  alikuwa Dkt Bashiru na wengi  wanafikiri mimi nimekuwa  tu kiongozi mimi ni zao la Dkt Bashiru  hivyo najivunia  chuo  hiki kuanza leo " 


Huku  Katibu  mkuu wa UVCCM Taifa Mwl Raymond Mwangwala  na mwenyekiti  wake Taifa Kheri James  nao  wakitumia jukwaa hilo kujipongeza kwa kuanza kwa   chuo  hicho  kuwa na jitihada  zao na wanapaswa kujipongeza  wenyewe  kwa kazi  hiyo kuwa .

Mwangwala  alisema chuo hicho  kinataraji  kuwa na miradi zaidi ya 21  na kuwa hadi sasa  chuo cha kushona  sare  mbali mbali kimeanza kwa msaada  mkubwa wa MNEC Iringa Salim Asas  aliyejitolea  kujenga jengo la chuo  hicho  na zaidi ya shilingi milioni 800 zimetumika hadi sasa  kati ya kiasi cha shilingi bilioni 22  zinazotarajiwa  kutumika  kujenga miradi  yote  chuoni hapo .
Share To:

Francis Godwin Mzee wa matukiodaima

Post A Comment: