Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma
Imeelezwa kuwa endapo jamii haitachukuwa hatua sitahiki dhidi ya magonjwa yasioyakuambukiza  zaidi ya dola za kimarekani trilioni 7 zitakuwa zimepotea ifikapo 2025 ambapo gharama hizo ni sawa na asilimia 4 ya pato la taifa kwa mwaka katika kipindi husika.
Takwimu zinaonesha kuwa asilimia 63 ya vifo vyote vitokanavyo vya magonjwa yasiyo ya kuambukiza hutokea kwa watu wenye umri chini ya miaka 70 katika nchi za kusini mwa jangwa la sahara wengi hufariki katika umri mdogo kulinganisha na nchi zilizoendelea ambapo tatizo hili huwapata watu wenye umri mkubwa.
Hayo yamebainishwa leo jijini Dodoma  na naibu waziri wa afya maendeleo ya jamii jinsia,wazee na watoto  Dkt faustine ndungulile katika kongamano la kwanza la kitaifa la udhibiti wa magonjwa yasioambukizwa, ambapo amesema kuwa magonjwa yasioyakuambukiza husababisha asilimia 34 ya vifo vyote vitokeavyo kusini mwa jangwa la sahara ambapo magonjwa ya moyo pekee husababisha asilimia 12 ya vifo vitokeavyo afrika mashariki.

Ameongeza kuwa magonjwa yasio ya kuambukiza yatokanayo na mfumo wa maisha tunayoishi ambao tunao  uwezo wa kuudhibiti, mathalani tabia ya uvutaji sigara, aina ya vyakula ambapo matumizi ya chumvi na mafuta mengi katika chakula ni sababu kuu ya magonjwa hayo.

Akieleza  lengo la serikali kuja na mkakati huo mkurugenzi wa tiba wizara ya afya Dr grace magembe amesema serikali inatumia gharama kubwa katika matibabu ya magonjwa hayo, ambapo awali magonjwa yakuambukiza ikiwemo kifua kikuu na ukimwi serikali imefanya kazi kubwa kuyapunguza nchini.

Nao baadhi ya wahanga wa magonjwa yasio yakuambiza katika kongamano hilo walilisisitiza jamii kuepukana na matumizi ya pombe ambapo Asilimia kubwa ya vijana ndio waathirika.
Kongamano la kwanza linalojadili udhibiti wa magonjwa yasioyakumbukiza limefunguliwa leo rasmi jijini Dodoma na naibu waziri wa afya dkt faustine ndungulile ambalo litahitimishwa tarehe 14, nov mwaka huu  ikienda sambamba na kauli mbiu isemaye “tutembee pamoja katika kudhibiti magonjwa yasio ya kuambukiza.


Share To:

msumbanews

Post A Comment: