;Mwanzilishi na Mkurugenzi wa Taasisi ya Elimu Afrika Daniel Urioh.Picha na Vero Ignatus.
 Baadhi ya wanafunzi wakiwa katika mafunzo ya kubadili Tabia na Uongozi yaliyofanyika hivi karibuni katika Shule ya Sekondari ya Connerstone iliyopo Ngaramtoni mkoani Arusha
 Wanafunzi waliohudhuria katika mafunzo ya Kubadili tabia na uongozi yaliyofanyika katika shule ya Sekondari Connerston wakishangilia baada ya mwenzao kuonyesha kipaji chake (hayupo pichani)
Wanafunzi waliohudhuria katika mafunzo ya Kubadili tabia na uongozi yaliyofanyika katika shule ya Sekondari Connerston wakifuatilia kwa makini kile kilichokuwa kinaendelea katika Mafunzo 


Na.Vero Ignatus,Arusha.

Ikiwa leo ni siku ya watoto duniani, jamii imetakiwa kuwajengea uwezo Watoto kuziishi ndoto zao na kutambua kuwa Watoto huanza Maisha pale wanapozaliwa hivyo kila hatua iwe wezeshi kwa watoto kufikia ndoto zao.

Limekuwa ni jambo la kawaida katika jamii kubwa za kiafrika ,wazazi au walezi kuwalazimisha Watoto wao kufikia ndoto ambazo wao hawajazifikia na haswa kwa kutumia mifumo rasmi kama ya Elimu ambayo inamuandaa mtoto kuwa kama jamii inavyotaka na siyo kama apendavyo yeye mwenyewe

‘’Utamsikia mzazi akimlazimisha mtoto wake kwa kumwambia nataka usome uje kuwa daktari,askaripolisi,Mwanajeshi,mwanasheria,mwalimu,bila kumsikiliza mtoto anapenda kuja kuwa nani ili aweze kumtilia mkazo Zaidi katika jambo lile alipendalo’’

Daniel Urioh ni Mwanzilishi na Mkurugenzi wa Taasisi ya Elimu Afrika amewaambia waandishi wa habari  kuwa wazazi wawe na muda wa kukaa na watoto wao, wapate kuwasoma, kujua vitu wanavyoelekea kuvipenda waanze kutilia mkazo ,ili waweze kuwakutanisha na watu ambao wamefanikiwa katika sekta hizo, ili kuwajengea hamasa za kufikia ndoto zao.

‘’ Mazingira ya mtoto huanzia nyumbani pamoja na wale wanaomzunguka,mifumo sikivu kwa ndoto za watoto siyo kuwafanya waishi kwa matakwa ya kile wanachokipenda wazazi , jambo ambalo linapelekea mtoto kukwama kufikia malengo yake pindi anapokuwa mtu mzima na kuanza kujitegemea’’alisema Mkurugenzi  

Ametoa wito kwa walimu ambao wananafasi kubwa katika Maisha ya Watoto, kuwa wapo nao muda mwingi Zaidi katika mazingira yao haswa shuleni kuliko mtu mwingine yeyote, watumie nafasi hiyo kulea ndoto, vipaji, ubunifu wawatoto hao kwa mbinu zisizodhalilisha,kuumiza au kuwakatisha tamaa (non-violence strategies)

‘’Baadhi ya walimu wamekuwa na tabia ya kuua ndoto, vipaji na ubunifu wa Watoto kwa lugha za kidhalilishaji,za kuumiza na kukatisha tamaa  Watoto jambo ambalo siyo zuri kabisa’’alisema Daniel.

Aidha katika kuadhimisha siku ya Watoto duniani Elimu ya Afrikainachukua jukumu la kuleta suluhu kwa kutumia programu na makongamano ya kuwatia moyo, kuwatengenezea majukwaa ya kujifunza na kuonyesha vipaji na bunifu zao.

Amesema kuwa  Vijana hupata nafasi kushirikiana kwa pamoja, kuhamasishana kuleta majibu ya changamoto zinazowazunguka na mwisho hutumia vipaji kuburudisha pia.

Siku ya watoto duniani  huadhimishwa kila mwaka duniani ambapo ilianzishwa na mwaka 1954 na husheherekewa tarehe 20 mwezi wa novemba kila mwaka kwaajili ya kuhamasisha na kueneza uelewa miongoni mwa Watoto duniani.

MWISHO.
Share To:

Vukatz Blog

Post A Comment: