Tuesday, 5 November 2019

WADAU WA MAJI NCHINI KUFANIKISHA MIRADI YA MAJI KWA UBORA KWA MANUFAA YA WANANCHI KWA KUTUMIA MBINU ZA KISASA ZA UPATIKQNAJI WA FEDHA.

Na Lucas Myovela_Arusha.

Naibu Katibu mkuu wa wizara ya maji Mhandisi Anthony Sanga Amezitaka taasisi na wadau wa maji zikiwemo mamlaka za maji nchini kutumia Fedha za wadau wa taasisi za kifedha kujenga miradi midogl na mikubwa ya maji lengo ni wananchi wapate huduma bora.

Akizungumza wakati wa ufunguzi ya warsha ya wadau wa mamlaka za maji wanao tegemea  ruzuku kutoka serikalini iliyo andaliwa na shirikisho la wadau wa usamabazaji wa maji nchi hapa nchini ATAWAS,Lengo likiwa ni uboreshaji wa upatikaniji fedha ili kuboresha huduma za maji hapa nchini.

Sanga ameleza kwamba sehemu ambapo serikali haijapeleka fedha zake ni vyema taasisi za kifedha za kuelekeza katika ujenzi wa miradi ya maji ili kukwamua hali ya ugumu wa upatikanaji wa maji kwa wananchi wanao kosa huduma za maji safi na salama na yenye kutosheleza.

"Wanachi wanataka kuona upatikanaji ya serikali haitokaa ikavumilia kuona mkandarasi anachezea pesa za walipa kodi kwasasa nguvu yetu kibwa ni kuzielekeza katika upatikanaji wa maji safi na salama kwa gharama nafuu na yenye ubora kwa wananchi sasa fedha hizi za wadau wa taasisi za kifeza niwaombe wazielekeze katika ujenzi wa miradi ya maji" Alisema Mhandisi Sanga.


"Mpaka sasa tuna jumla ya miradi 1947 tunayo ijenga nchi nzima pamoja na kuwa ma changamoto mbali mbali hapo mwanzo kutokana na upatikanaji wa wakandasi na chini ya usimamizi mzuri lakini kwa awamu hii ya tano inayo ongozwa na Rais Magufuli inashugulikia wakandarasi wote ambao wanajenga chini ya kiwango na sisi kama wizara kwasasa tunawashibiti vyema wakandarasi pamoja na miradi yao". aliongeza Mhandisi Sanga.

Awali akiongea na waandishi wa habari mkurugenzi mwendeshaji wa taasisi ya wadau wa huduma za maji nchini (ATAWAS) Ndg Costantino Fidelis amesema kuwa uhaba wa maji unatokana na ukosefu wa fedha za ujenzi wamiradi ya maji ndio maana wameamua kuwajengea uwezo watendaji wa mamlaka za maji ngazi ya mikoa kupitia mafunzo ya kuombea fesha za miradi kutoka kwenye taasisi za kifedha kuweza kutekeleza upatikanaji wa miradi ya maji hapa nchini.


Alisema kuwa hayo ndio yamewafanya kuona umuhimu wa kuendesha warshahiyo ili kuona miradi ya maji ikitekelezwa na kuondoa uhaba wa uhaba wa maji hapa nchini ikiwemo ikiwemo swala zima la upatikanaji wa fedha kwa lengo la kumtua mama ndoo kichwani. 

"Matarajio ni kufungua milango kwa mamlaka za maji kuwa na fedha za kutosha kutekeleza miradi ya maji nchini ambayo itasaidia kuondoa 
uhaba wa majikwa wananchwengi zaidi hivyo kufikia malengo yaserikali” alisema Fidelis.
Nae kwa upande wake Afisa Mwendeshaji wa Kiwanda cha kutengeneza mabomba ya maji ya plastiki ( PLASCO LTD ) Bw Alimiya  Osman ameeleza kwamba wao kama wadau wakubwa wa maji kwa kutengeza mabomba imara ya plastiki duniani katika kuhimili,kuhifashi na kupitisha maji pasipo kuharibika.


Bw Alimia amesema kuwa kufuatia teknologia mpya waliyo ileta hapa nchini kwa mara ya kwanza kutoka  nchini Finland,Teknolojia hiyo inawasaidia kutengeneza mabomba  ya plastiki ya maji taka yenye mita 2.2 pia teknolojia hii itakumika kutengeza mabomba ya maji safi ambayo ni imara zaidi duniani.

"Mbali na bidhaa zetu pia tumekuchuja kusikiliza changamoto za wadu wa maji kwani sisi pia ni wadau wakubwa wa maji hapa nchini ili kiweza kijua uhitaji wao wa bomba za maji kutoka na uhitaji uliyopo hapa nchini kufuatia miradi mingi inayo jengwa ili kuweza kukuza uchumi wetu wa viwanda hapa nchini na wao pia waelewe kiwanda kikubwa kama chetu kinafanya kazi na wadau kama wao ambao ndiyo wateja wa bidhaa zetu" alisema Alimia

"Ili kuweza kufanikisha swala la utoaji huduma tunaomba serikali na wadau wa maji kuangalia matumizi ya fedha wanazo pata kununua bidhaa bora za mabomba kutoka katika kiwanda chetu cha nyumbani ili kuongeza uchumi na kupunguza tatizo la ajira hapa nchini kwanibitachangia kwa kasi kubwa ukuaji wa viwanda vya ndani kuendana na kasi ya serikali ya awamu ya tano ya Tanzania ya viwanda".alisema Osman.

No comments:

Post a Comment