Wednesday, 20 November 2019

CCM KIMANGA WAZINDUA KAMPENI KWA KUTAMBULISHA WENYEVITI WAKENA HERI SHABAN

CHAMA cha Mapinduzi CCM Tawi la Kimanga Darajani wamezindua kampeni za Uchaguzi za Serikali za Mitaa kwa kupita mitaani kuwatambulisha Wenyeviti wa Chama chao .

Chama hicho cha  Mapinduzi Tawi la Kimanga darajani walayani Ila─║a kiliwatambulisha wenyeviti wake Mitaani wagombea wote wakiwemo Wenyeviti wa Serikali za Mitaa waliopita bila kupingwa.


Akizungumza katika uzinduzi huo Mwenyekiti wa CCM wa Kimanga Darajani wilayani Ilala  Ephrahim Makoye alisema dhumuni la Chama cha Mapinduzi kuendelea kushika dola  na kutumikia wananchi wake kwa kutekeleza Ilani ya Chama.

"CCM Kimanga darajani leo tumewatambulisha Wenyeviti wa Serikali wa Mitaa yote mitatu pamoja na Wajumbe wake,mtaa wa Sokoine,Twiga  na Kimanga darajani leo wananchi wawatambue na wawe na imani na chama chao"alisema Makoye.

Makoye alisema  CCM kwa sasa ndio chama kilicho madarakani ,kitaendelea kuwa madarakani amewataka Wenyeviti watarajiwa wa Serikali za Mitaa waliopata fursa kushiriki katika uchaguzi mwaka huu wasimamie misingi ya chama na kutekeleza Ilani ya chama katika kutumikia wananchi.


Makoye alisema asiyekubali kushindwa sio mshindani vyama vya upinzani vimeishiwa sera hawakutakiwa kugomea uchaguzi na chama cha Mapinduzi akijawai kushindwa hata siku moja.

 Alisema CCM imejipanga vizuri mikakati yake  mwakani itaendelea  kushika dola kwa kuchukua majimbo yote .

Aidha alisema Rais John Magufuli amefanya   mambo makubwa katika  kujenga Tanzania ya Uchumi wa viwanda   amewataka  Wagombea wa Wenyeviti wa Mitaa na Wajumbe wake kuunga mkono juhudi za Rais na kuendeleza mazuri katika kusimamia miradi ya maendeleo na kulinda rasilimali za nchi.

 Kwa upande wake  Mgombea wa nafasi ya Mwenyekiti wa Mtaa wa Sokoine Sharifa Orembe alisema katika uongozi wake atakapokuwa madarakani atashirikiana na Wananchi wake katika kutatua changamoto na katika kujenga Mtaa wa Sokoine na Kimanga kwa ujumla.

Sharifa alisema pia atawawezesha vijana na Wanawake katika Shughuli za kukuza uchumi na ujasiriamali ikiwemo kusimamia sekta ya elimu na kuongeza ufaulu Kata ya Kimanga kwa kukuza taaluma.

MWISHO

No comments:

Post a comment