Na Lucas Myovela_ARUSHA.

Timu ya Netball ya jiji la Arusha (Arusha Queen's ) imetwaa nafasi ya 3 ya ushindi katika michuano ya Ligi kuu ya Netball Tanzania yaliyo kuwa yakifanyika jijini Dodoma.

Mashindano hayo ya Ligi kuu ya Netball  yaliyo shirikisha timu 10 kutoka Tanzania bara yamemalizika huko jijini Dodoma na Arusha Queen ikiibuka kidedea na fasi ya tatu kwa mara ya kwanza baada yaa kushiriki michuano hiyo kwa miaka mitano mfululizo.

Katika michuano hiyo kwa muda mrefu timu kongwe ziliweka rekodi ya kuto kutolewa katika msimamo wa ushindi wa tatu bora lakini kwasasa timu ya Arusha Queen's imeanza kuvunja rekodi hiyo ya kuwatoa wababe wa muda mrefu katika mashindano hayo ya mpira wa Netball.

Benson Maneno ni Afisa utamaduni wa Jiji la Arusha yeye ameeleza kuwa ushindi huo wa Arusha Queen's umekuja wakati muafaka kutokana na mikakati ya muda mrefu wa kuinoa timu hiyo ili iweze kuchukua ushindi mbali mbali hapa nchini na hata Africa Mashariki na kati.

 "Kwa kufuatia ushindi huu wa tatu katika michuano hii ni nafasi kubwa kwetu na inatia hamasa toka tulivyo anza kushiriki mashindano haya timu nyingi zinazo mikikiwa na majeshi ya polisi hapa nchini ndiyo zilikuwa zikuchukua ushindi pekee hasa katika nafasi tatu bora lakini sasa tunawahakikishia watanzania Arusha Queen's kwa ujio wake huu tunatazamia mambo makubwa hasa kuchukua ubingwa na ushindi mbali mbali hapa nchini na nje ya Nchi" alisema Benson Maneno.

"Hata hivyo timu kwasasa inajipanga kwaajili ya kushiriki na kuchukua ubingwa katika michuano ya kombe la Muungano inayotarajiwa kufanyika zanzibar mwezi december mwaka kuu na kikosi tayari kimesha anza kunolewa kwa kasi ya juu sana kuhakikisha hatutopoteza mchezo hata mmoja katika mashindano haya na kuibuka wa shindi wa kwanza katika kombe la mungano mjiji Zanzibar". aliongeza Maneno

Kikosi cha Arusha Queen's kilichopo chini ya kocha mahiri kutoka nchini uganda Nurdin Hassan kimeweka kambi jijini Arusha kuendelea kujifua kuhahikisha kinachukua kombe la Muumgano huko Zanzibar,huku pia ikiendelea kusajili wachezaji wapya kuhakikisha kikosi kinakuwa imara na kabambe.

Nae kocha wa Arusha Queen's Nurdin Hassani ameeleza kwamba mafunzo anayoyatoa kwa kikosi hicho ni kuchukua ubingwa na siyo kushiriki mashindano na kuongeza kwamba moshi tayari umeanza kuvuka kwa kuchukua na fasi ya tatu michuano ya Netball Tanzania na kujihakikishia ubingwa katika kombe la Muungano mwishinoni mwa mwaka huu.

Kwa upande wa wadau wa mchezo wa Netboll jijini arusha wameipongeza timu ya Arusha Queen's kwa mafanikio hayo makubwa ya mwanzo kwa ushindi wa 3 waliyo upata katika michuano ya Ligi kuu ya Netboll Tanzania.
Share To:

Lucas Myovela

Post A Comment: