Mwenyekiti wa Jukwaa la Wanawake Kivule Pasikazi Machaga akipatana bei na Mgeni rasmi Katika uzinduzi wa jukwaa la Kivule Makamu Mwenyekiti wa Jukwaa wilaya ya Ilala Sauda Addey na Mratibu wa Dawati la Jukwaa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Georgis Asenga leo. 
Mratibu wa Dawati la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Wilaya ya Ilala Georgis Asenga (Katikati)akiangalia bidhaa za Maonesho ya Wajasiriamali wa Kata ya Kivule manispaa ya Ilala , wakati wa Uzinduzi wa Jukwaa lao leo ,(kushoto )mgeni rasmi Makamu Mwenyekiti wa Jukwaa wilaya ya Ilala Sauda Addey na Mwenyekiti wa Jukwaa Kivule Paskazia Machaga
Mgeni rasmi Makamu Mwenyekiti wa Jukwaa la Wanawake Wilaya ya Ilala Sauda Addey akiangalia bidhaa za maonyesho, katika uzinduzi wa Jukwaa la Wanawake wa Kata ya kivule Manispaa ya Ilala leo,(Kulia )Mratibu wa Dawati la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Wilaya ya Ilala Georgis Asenga ,na Ofisa Mtendaji wa Kivule(PICHA NA HERI SHAABAN)


NA HERI SHAABAN

HALMASHAURI ya Manispaa ya Ilala imesema wananchi wake waliopo ngazi ya Kata wapewe ushirikiano ili waweze kupewa  mikopo Ofisa  atakayewasumbua na kuweka vikwazo atolewe taarifa ili hatua ziweze kufuata.

Hayo yalisemwa na Mratibu wa Dawati, Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Wilaya ya Ilala Georgis Asenga wakati wa ufunguzi wa Jukwaa la Uwezeshaji wananchi Kiuchumi Kata ya Kivule ambapo mgeni rasmi alikuwa Mwakilishi kutoka kwa Mkuu wa Wilaya  Ilala,Makamu Mwenyekiti wa Jukwaa Wilaya ya Ilala Sauda Addey.

"Waombaji mikopo wote kutoka katika Mitaa na Kata wapewe ushirikiano ili waweze kupata mikopo wasipewe usumbufu  mkisumbuliwa mje Halmashauri kwani mikopo ni yenu akuna mtu atakayeweka vikwazo "alisema Asenga .

Asenga aliwataka waombaji mikopo wafute taratibu kuanzia serikali ya Mtaa  na mikopo kwa upande wa vijana wambatanishe na vitamburisho ili watamburike umri wao wasipewe waliopitiliza umri kwa upande wa mikopo ya Vijana inayotolewa ngazi ya halmaashauri ya Wanawake,Vijana na Watu wenye Ulemavu.

Alisema katika kata ya Kivule vikundi 20 vishapewa mikopo bado vikundi 11 vipo katika utaratibu wa kupata mikopo hiyo alimwagiza Diwani wa Kivule kupitisha vikundi sahihi kutoka katika kata hiyo.

Halmashauri ya Ilala inatoa mikopo ya Serikali kupitia ngazi ya halmashauri imeshatoa awamu mbili awamu ya tatu mwezi Juni mwaka huu  itatolewa , mikopo mbalimbali kwa mujibu wa Mkurugenzi wa halmashauri ya Ilala , alisema awamu ya tatu watatoa Bajaj 50 Bodaboda 50 na mikopo ya magari kwa vikundi.


Kwa upande wake Mgeni rasmi Makamu Mwenyekiti wa Jukwaa wilaya hiyo Sauda Addey alisema Jukwaa ni utekelezaji wa Ilani ,pia ni sehemu ya fursa.

Sauda alimwagiza Diwani wa Kivule kuwapa ofisi katika ofisi ya Kata kwani Jukwaa ni la serikali  wakati wakitafutiwa eneo la kuwapa ofisi kwa ajili ya shugjuli zao.

Aidha pia  alimwagiza Diwani wa Kivule kuwasimamia Wanawake wa Kivule waweze kupata tenda ya Usafi katika hospitali ya Wilaya ya Ilala inayotarajia kukamilika mwezi Juni 2019

Aliwataka Wanawake kujitambua na mikopo watakayopata watumie kwa dhumuni lililokusudiwa ikiwemo ufunguaji wa viwanda vidogovidogo.

Naye Mwenyekiti wa Jukwaa la Uwezeshaji wananchi Kiuchumi kata ya Kivule Paskazia Machange alisema    Kivule ina mtaa wa Kerezange,Mtaa wa Bombambili ,Mtaa wa Magole na Kivule wanawake wote wameunganishwa katika jukwaa hilo  lenye jumla ya Wanawake 2750  vikundi 170 vyote vimesajiliwa  .

Mwenyekiti wa Kivule Paskazia alitoa ombi kwa Serikali ya Wilaya ya Ilala wapewe fursa za kufanya usafi hospitali ya Kivule pamoja na kupata tenda ya zabuni ya Chakula mara hospitali ya wilaya ya Ilala itakapokamilika  vifaa wanavyo.

Mwisho
Share To:

msumbanews

Post A Comment: