Tuesday, 30 April 2019

Breaking : Mwenyeviti watano wa Vijijini Arumeru Watimkia Ccm


Baada ya kumtuhumu Mkuu wa wilaya ya Arumeru ndugu Jerry Muro kuamuru kushushwa kwa bendera za chadema, sasa Wenyeviti wa vijiji vitano na vitongoji viwili wa kata ya songoro Halmashauri ya Meru Wilayani Arumeru wameamua kukihama chama cha Demokrasia na Maendeleo chadema na kujiunga na ccm kwa lengo la kumuunga mkono mkuu wa wilaya ya Arumeru katika harakati zake za kuleta maendeleo. 

Ambapo Wenyeviti wa Vijiji Vitano wa Chadema kata ya Songoro halmashauri ya Meru wamekihama chama hicho na kujiunga na CCM wakati wa mkutano wa hadhara wa Mkuu wa wilaya ya Arumeru Ndugu Jerry Muro katika kata ya Songoro.
Walirudi CCM ni Bw Eliah Mathayo Mbise mwenyekiti wa kijiji cha Songoro, Bw Pokeali latiaeli Nnko wa kijiji cha mulala, Bw Sadikiel Solomon Ayo wa kijiji cha Sura pamoja na Bw Elifasi sunguroi Nassari wa kijiji cha Kilinga.

Pia wamo wenyeviti wawili wa vitongoji Bw Anathe Eliah mbise kitongoji cha meto kijiji cha mulala, pia Sinyaeli ndetaulo mbise wa kitongoji cha kiuta kijiji cha songoro 

Pamoja na hao ni katibu mwenezi wa chadema kata ya Songoro Bw George peter Pallangyo pamoja na mwenyekiti wa Bawacha Bi Ekael felix 

Kwa sasa kata ya Songoro vijiji vyote sita vimerejea chama cha mapinduzi 

#ArumeruYetu #WakatiWetu #CCMYETU

No comments:

Post a comment