Wednesday, 20 March 2019

Mambo makuu mawili yanayokufanya uendelee kuwa maskini


Habari za muda huu mpenzi msomaji wa blog ya www.Msumbanews.co.tz bila shaka u mzima wa afya  na unaendelea vyema na majukumu yako ya kila siku. Naomba nichukue walau dakika zako kadhaa kuweza kukuja mambo makuu mawili ambayo yatakufanya uendelee kuwa maskini endapo utaendea kuyang’ang’ania. Na mambo hayo ni;

1. Kutenda bila kufikiri.
Wapo baadhi ya watu wanashindwa kufikia katika kilele cha mafanikio yao hii ni kwa sababu watu hao hawataki kujitoa kwa moyo wote katika kufanya vitu ambavyo wanafanya. Hata wale wanaojitoa kwa moyo vile vile huwa wanafanya vitu hivyo pasipo kufanya uchunguzi wa kina juu ya mambo ambayo wanayafanya.

Watu hawa ndio wale ambao utakuta wanatumia nguvu nyingi kuliko kuishirikisha akili, na kitendo hiki ndicho watalamu wa masuala ya mafanikio huita msuli tembo matokeo sisimizi, yaani watu hao hujikuta vitu mbalimbali ilimladi wameafanya.

Na ukweli ni kwamba katika kundi hili kuna watu wengi sana ambao wamejikusanya kwa pamoja katika kundi hili na hawa ndio wale wanaongoza kwa kusema vyuma vimekaza, nami nasema ya kwamba  kama na wewe upo katika kundi hili na hutaki kubadilika ninasema utapata tabu sana.

Nisikutishe kwa maneno ya msingi bali unacahotakiwa kufanya katika maisha yako ili uweze kufanikiwa ni kuhakikisha kwa kila jambo unalotaka kulifanya au ambalo unalifanya ni kuhakikisha unatenda jambo kwa kuwekeza fikra zako katika jambo hilo. Hiiitakusadia sana kujua mchakato mzima wa jambo hilo matokeo yake kiujulma.

2. Kufikiri bila kutenda.
Mtafiti mmoja kutoka chuo cha kikuuu cha harvard nchini Marekani aitwaye Sabrina Deogratius yeye aliwahi kusema ya kwamba kufikiri bila kutenda ni mawazo ya mtu mfu, hii ikiwa ni sawa na kusema nataka kufanya jambo fulani bila kuchua hatua stahiki ya kutenda jambo hilo haya huwa yanaitwa ni matamanio tu.

Na katika kundi hili la watu wenye matamanio limebeba idadi kubwa sana ya watu, na watu hao ndio wale wenye utajiri sana wa meneno ila ndio maskini wa kutupwa, wao vinywa vyao hujaa ahadi zisizotekelezeka. Watu hao ndio wale wenye kuamini vitu ambavyo havipo, utakuta hata ukitaka kuwashirikisha jambo fulani la kimaendeleo watakwambia jambo hilo haliwezekani hii ni kwa sababu wao huishia kuwaza tu na si kufanya.

Hivyo ndugu yangu maisha yanakwenda kasi sana hivyo yakupasa nawe uweze kuendana na kasi hiyo kwa kuhakikisha ya kwamba kila unalolifikiri kama ni jambo lenye manufaa kwako na jamii ambayo inakuzunguka ni vyema ukahakikisha unalifanya kwa kina.

Kwa nukta hiyo kwa leo sina jambo la ziada nikutakie siku njema na mafanikio mema.

Na: Benson Chony

No comments:

Post a comment