Wednesday, 11 July 2018

Mwenyekiti wa Chadema Arusha Atimkia Ccm na Wanachama zaidi ya 40

Mwenyekiti wa Mtaa wa Olmatejo B katika kata ya Sakina Jijini Arusha Ndg.Eluicent  Lembris  mapema leo hii ameamua kujiuzulu nyadhifa  zake zote na kujiunga na Chama cha Mapinduzi Ccm  akiwa ameambatana na wanachama zaidi ya Arobaini. (40)
Mwenyekiti wa Ccm Wilaya ya Arusha Ndg. Joseph Masawe Akimpokea aliyekuwa Mwenyekiti wa Mtaa wa Olmatejo B kwa tiketi ya Chadema mapema hii leo alipojiunga na Ccm.
Wanachama wapya waliopokelewa wakiwa na Viongozi wa Ccm Wilaya ya Arusha nje ya Ofisi za Ccm Wilaya.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Ccm katika Kata ya Sakina Bi.Neema Mollel Akizungumza Mara baada ya kupokelewa kwa wafuasi wa Chadema zaidi ya Arobaini  (40) waliojiunga na Ccm kutoka kata ya Sakina Mkoani Hapa.

No comments:

Post a comment