Friday, 13 July 2018

Makamu Mwenyekiti NCCR-Mageuzi(Bara) Ajiunga na CCMMakamu Mwenyekiti wa chama cha NCCR-Mageuzi (Bara), Leticia Mosore leo Ijumaa Julai 13, 2018 ametangaza kujiunga na CCM

Amejiunga pamoja na wanachama wengine watano, akiwemo aliyekuwa mjumbe wa halmashauri kuu ya chama hicho, Mchata Mchata

Amesema "Kinachonikera kwenye upinzani ni kupinga kila kitu hadi mazuri wakati hayo ndio tulikua tunayasema, mpaka mwisho hatueleweki tunataka nini, Hivyo mtu mzima kama mimi nimeona bora nirud CCM"

"Niliamua kuhama CCM sababu utekelezaji wa ilani haukuwa wa kuridhisha, rushwa na ukosefu wa maadili vilikithiri. Upinzani wa wakati huo walisimamia hoja hizi, zilinigusa nikashawishika kuungana nao ili tunusuru nchi".
 
Credit Jf

No comments:

Post a Comment