Baada ya ukimya wa wiki moja, Casto Dickson Jumatato hii amepost picha yake ya kwanza ikawa ni siku 4 toka mtoto wa Muna, Patrick Peter ambaye alikuwa akidaiwa ni wake azikwe katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es salaam.
Mtangazaji huyo wa kipindi cha Siz Kitaa cha Clouds TV, hakuweza kuzungumza chochote wala kuonekana toka msiba huo utokee licha ya aliyekuwa mpenzi wake, Muna kudai mtoto huyo alikuwa ni wake na sio wa Peter Komu ambaye alikuwa mume wake wa ndoa.
Kauli hiyo ya Muna iliwasha moto upande wa familia ya Peter ambapo ilidai kwamba itakwenda mahakamani kama mrembo huyo asingekubali kutoa mwili wa mtoto huyo ili wamzike kwa kuwa ni mtoto wao na wanavielelezo vyote.
Baada ya kauli hiyo Muna ambaye alikuwa nchini Kenya pamoja na mwili wa marehemu, aliamua kukubali kutoa mwili wa mtoto huyo na kushirikiana na familia ya Mzee Peter kwaajili ya mazishi na kuzikwa Jumapili hii katika makaburi ya Kinondoni.
Kupitia Instagram, Casto amepost picha yake ya kwanza na kuonyesha kumshukuru Mungu, lakini picha hiyo imevuta hisia mpya kwa wasanii pamoja na wadau huku wengi wakimpongeza mtangazaji huyo kwa kuamua kukaa kimya kipindi chote cha matatizo.

Maoni wa wadau hao pamoja na wasanii.
Petermpangala16
Kaka hakuna kama wewe kweli nimeamin ukubwa dawa.

Gipcegapson

Dah pole sana brow kwa mambw uliyopitia ila kama Mwanaume umejikaza na umesimama tena Mungu yuko upande wako.. Big up sana.

Kisura_04

Nimependa sana @castodickson hongera kwa kuvumilia ukimya ni busara kubwa kwa nyakat ngum kama ulizoptia keep t mr yu will speakout when yu think is the right time.
Adamchomvu
Means life ma nigger…worry not sisi ndio binadamu matatizo ni yetu.
eduboytz
Mfano wa kuigwa.
Missmandoza
God is good 🙏🏾
Siku mbili kabla ya kifo cha Patrick, Casto alihojiwa na Clouds TV na kumlaumu Muna kutomuhusisha kwenye ishu za kuugua kwa mtoto huyo ambaye alikiwa anasumbuliwa na uvimbe kichwani.
Alisema hayo baada ya Muna kuonekana kuangaika peke yake kuhusu matibabu ya mtoto wake huyo.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: