Saturday, 14 July 2018

Breaking News: Rais Magufuli Katengua uteuzi wa Mkurugenzi wa NSSF

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ametengua uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF)Prof. Godius Kahyarara kuanzia leo July 14, 2018. Prof. Kahyarara atapangiwa kazi nyingine.

Kufuatia hatua hiyo, Rais Magufuli amemteua William Erio kuwa Mkurugenzi Mkuu wa NSSF.

Kabla ya uteuzi huo Erio alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF. Uteuzi wa Erio unaanza leo July 14, 2018.

No comments:

Post a Comment