Friday, 1 June 2018

Ferooz : Nataka niache muziki lakini najikuta nashindwa

Msanii mkongwe wa Bongo Flava, Ferooz amesema kuwa kuna wakati anatamani kuacha muziki lakini anashindwa.

Muimbaji huyo ameeleza sababu ya kutaka kufikia uamuzi huo ni kuonekana si kitu wakati ameutoa mbali muziki huo.
“Kikubwa kinachoniumiza nikiangalia game nilipolitoa mpaka lilipofika halafu bado naonekana mimi ndio nimekosea, mkosefu namba moja,” amesema.
“Game linanisahau kwa kifupi, mkapa nafikia fikra za kusema ni quit kufanya muziki, ni quit kufanya game, nitangaze nimeacha muziki. Nataka niache muziki lakini najikuta kwamba nashindwa kwa sababu imeshakuwa kwenye damu,” Ferooz ameiambia Wasafi TV.
Ameongeza kuwa licha ya kufanya muziki kwa takribani miaka 20 sasa amekuwa pia akifanya mambo mengine lakini mwisho wa siku anajikuta amesharudi kwenye muziki. Wimbo wa mwisho kutoa Ferooz unakwenda kwa jina la Najaribu

No comments:

Post a comment