Saturday, 12 May 2018

Mbunge Lema aichambua kazi ya Bunge

Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema (CHADEMA) amesema kazi ya Bunge ni kuisimamia serikai.
Lema, leo Mei 12 amedai kuwa Tanzania kazi ya Bunge ni kusimamiwa na serikali huku akiwata wananchi kuelewa hivyo.
“Kazi ya Bunge ni kuisimamia Serikali,Tanzania kazi ya Bunge ni kusimamiwa na Serikali,hivi ndivyo wananchi wanapaswa kuelewa,Bunge ambalo haliwezi kusimamia haki ya Mbunge aliyepigwa risasi kupata haki yake,bunge hilo halitaweza kujua shida zenu za maji hata kama mnakufa na kiu,” ameandika Lema kupitia mtandao wake wa Kijamii.

No comments:

Post a comment