Tuesday, 29 May 2018

DIAMOND AFUNGUKA KUMWANGUKIA ZARI


Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’
AMEFUNGUKA kwa mara ya kwanza! Baada ya kusambaa kwa maneno ya chinichini kwamba mkali wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ amemuangukia mzazi mwenzake, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ akimuomba radhi ili warudiane, staa huyo ameibuka na kutolea ufafanuzi ishu hiyo.
Ubuyu huo uliosambaa kwa kasi kwenye mitandao ya kijamii, uliibuka hivi karibuni na kueleza kuwa, kwa nyakati tofauti, Diamond alitinga nchini Afrika Kusini ‘Sauz’, nyumbani kwa mwanamama huyo wa Kiganda na kumuomba msamaha ili waweze kurudiana na kulea watoto wao wawili, Tiffah na Nillan.
ETI NI KWA SABABU KAMKOSEA…
Ubuyu huo ulikolezwa nakshi mitandaoni baada ya kuaminika kuwa, Diamond ndiye mwenye makosa ndiyo maana Zari alitangaza kumuacha.
KWA NINI ZARI ALIMUACHA?
Mara kadhaa Zari amekuwa akieleza wazi kwamba, kilichomsababisha aamue kummwaga Diamond ni kutokana na kutokuwa mwaminifu na kuhisi anamkosea heshima.
MAHOJIANO ‘KARENTI’
Kwenye mahojiano yake ya hivi karibuni ‘karenti’ jijini Nairobi, Kenya, Zari alisema kuwa, aliamua kumpiga chini Diamond kutokana na matendo yake maovu (michepuko) na kamwe hayuko tayari kurudiana naye.Alisema kuwa, ataendelea kubaki kuwa baba wa watoto wake, lakini uhusiano wao hauwezi kufufuka upya kwa sababu ya usalama wake.

No comments:

Post a comment