Katibu wa Itikadi na Uenezi Taifa CCM, Humphrey Polepole ameagiza wasimamizi wa Mpango wa kunusuru kaya masikini na zenye upungufu wa chakula TASAF mkoa wa Arusha kufanya tathmini na kuongeza ruzuku kaya zinazofanya maendeleo ili kuongeza uzalishaji wenye tija
Akiwa katika ziara ya kikazi ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo ya TASAF ambayo ni sehemu ya utekelezaji wa ilani ya CCM Polepole amesema, kuwa ni vyema kuwaongeza ruzuku kwa kaya zinazoonesha matokeo chanya katika uzalishaji ili kuweza kuwa chachu ya maendeleo katika jamii.
"Mpango wetu sisi ni kuwavusha watanzania kutoka hali waliyonayo sasa na kwenda katika hali nzuri zaidi ifikapo mwaka 2020 ndiyo maana tunalipendekeza hilo. Lakini niwapongeze watu wa Arusha kwani nimeona miradi mingi ambayo itawafanya mtoke kwenye utegemezi," Polepole
Akisoma taarifa ya utekelezaji wa miradi mbalimbli mkurugenzi wa jiji la arusha Athumani Kihamia amesema asilimia kubwa ya kaya maskini hizo tayari wamesha patiwa kadi kwa ajili ya matibabu (Tika) yenye uwezo wa kuhudumia kaya sita kwa kadi moja.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: