Mwezeshaji  wa mafunzo ya Sayansi na teknolojia katika kituo cha  Sayansi cha Stem Park Shaukatali Hussein  akiwafundisha wanafunzi wa shule za msingi  na sekondari  katika kituo hicho wakati  wa maadhimisho ya wiki ya ubunifu mkoani Tanga
Mwezeshaji  wa mafunzo ya Sayansi na teknolojia katika kituo cha  Sayansi cha Stem Park Shaukatali Hussein  akiwafundisha wanafunzi wa shule za msingi  na sekondari  katika kituo hicho wakati  wa maadhimisho ya wiki ya ubunifu mkoani Tanga
Wanafunzi wa shule za msingi  na sekondari  wakifuatilia mafunzo hayo katika kituo hicho wakati  wa maadhimisho ya wiki ya ubunifu mkoani Tanga


NA OSCAR ASSENGA,TANGA.

ZAIDI ya  Wanafunzi  wapatao elfu nne '4000' kutoka shule za Msingi na Sekondari zilizopo ndani ya mkoa wa Tanga  pamoja na wale waliomaliza na walio nje ya mfumo wa elimu wameendelea kunufaika na mafunzo ya Sayansi  kwa vitendo yanatolewa na kituo cha Sayansi cha Sterm Park kwa lengo la kuwaongezea uelewa ikiwa pia ni njia ya kuwawezesha  kujiajiri kidijitali.

Hayo yamebainishwa na Meneja wa kituo hicho Max George wakati wa maadhimisho ya wiki ya ubunifu hapa nchini kwa mkoa wa Tanga ambapo kupitia kituo hicho wanafunzi wa ngazi tofauti na vijana waliohitimu masomo kidato cha nne na waliopo nje ya mfumo wa elimu  wamekuwa wakinufaika  .

George alibainisha kuwa kumekuwa na changamoto kwa baadhi ya Vijana ambao wapo nje ya mfumo wa elimu pamoja na wale ambao wameshamaliza elimu ya kidato cha nne kujiendeleza kielimu  ambapo katika kuhakikisha nao wanapata elimu  hiyo kwao vitendo wamefanya utaratibu wa kuwaingizia kwenye mfumo rasmi.

"Mpaka sasa tunashukuru muamko wa vijana ni mkubwa  na tumekuwa tukifanya kazi na shule zote za Jiji la Tanga ambapo tumeingia kwenye mfumo rasmi ambao unatuwezesha sisi na walimu kufanya kazi  kuwa pamoja , wao wakiwa wanaofundisha kwa nadharia sisi tunafundishwa kwa vitendo na  mpaka sasa wanafunzi wapatao elfu nne wamenufaika na mafunzo tunayotoa" alisema George.

 Aliongeza kuwa  kutokana jiographia ya mkoa wa Tanga ili kuwafikia wanafunzi wengine waliopo wilaya nyingine wamekuwa wakizitembelea ili kuhakikisha elimu hiyo inawanufaisha vijana wengi zaidi na kuondokana na tatizo la ajira ambalo limekuwa ni changamoto wa kundi kubwa la vijana.
hapa nchini, 

" Changamoto ni kwa vijana ambao wapo nje ya elimu na ambao hawajabahatika kabisa kwenda shuleni lakini kituo kinawahudumia katika kuwapa mafunzo ya program mbalimbali za kompyuta maeneo mengine nje ya jiji la Tanga tunafanya utaratibu kutembelea  shule kwaajili ya kuwapa elimu hii" alisema Meneja huyo.

Kwa upande wake  meneja wa mradi wa Project Insipire unaohamasisha kujifunza masomo ya sayansi  katika kituo hicho Dkt Issaya Ipyana aliwataka wanafunzi wa kike kupenda masomo ya sayansi na kuachana na dhana ya kuyaona masomo hayo ni magumu.

Dkt Ipyana alisema kuwa wazazi  na walezi wanazidi kuhamasika kwa kuwaleta watoto wao kujifunza katika kituo hicho huku akiongeza kuwa  kama wanafunzi wa kike wakipewa mbinu mapema za kuyajua masomo ya sayansi inaweza kuwasaidia kuipenda sayansi na kuwasaidia kwenye maisha yao ya baadaye. 

"Dunia inaelekea kwenye mlengwa wa Sayansi na Teknolojia na mtoto wa kike ana nafasi kubwa hivyo tukiwapa nafasi kujifunza masomo ya Sayansi itawasaidia mbeleni tofauti na sasa walivyo kwenye jamii" alisema Dkt Ipyana.

"Sasa tunaelekea ulimwengu wa Sayansi na kidigital hivyo kupitia mafunzo haya tunawajengea uwezo walimu pamoja na wanafunzi kupata uwezo na kujua kuwa kuna fursa kupitia ulimwengu wa utandawazi ambazo zinaweza kuwa njia ya kujiajiri"  aliongeza

Kwa upande wao wanafunzi akiwemo Sarah Michael na Hatuna Iddi wanaoshiriki programu hizo walisema kuwa  zinawapa mwanga na kuwawezesha kuyapenda masomo ya sayansi huku wakiwaomba wazazi na walezi kuwawezesha kuwapatia vifaa vya kujifunzia ili kuwaongezea uelewa zaidi. 

Hatua hiyo inafuatia wimbi la watoto wa kike kukimbia masomo ya sayansi jambo ambalo linawafanya wadau mbalimbali kuona umuhimu wa kuwekeza kwenye eneo hilo ili jamii iachane na hofu ya kujifunza masomo hayo. 

MWISHO.

Share To:

TANGA RAHA BLOG

Post A Comment: