Wadau kutoka Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania THRDC, wakiongozwa na mwenyekiti wa Bodi ya mtandao huo, Jaji Mstaafu, Joacquine De Melo, aliyeambatana na Mratibu THRDC, Onesmo Olengurumwa, mjumbe wa bodi ya mtandao, na Mkurugenzi wa ANGOZA kutoka visiwani Zanzibar, Hassan Juma, Mratibu wa THRDC kanda ya kati na mkurugenzi wa taasisi ya PLAJC, Bw. Jaruo Karebe, Mwakilishi kutoka THRDC-Zanzibar Bi. Shadida Omar, Wakili Nuru Maro, Afisa Uchechemuzi kutoka THRDC  Bi. Neema mwakilishi kutoka taasisi ya WOWAP, kwa pamoja  wametembelea Wizara ya Katiba na Sheria na kukutana na Waziri George Simbaachawene ambaye ameteuliwa kushika nafasi hiyo baada ya aliyekuwa waziri wa wizara hiyo, Prof. Palamagamba Kabudi.


Kwa upande wa Wizara, kikao hicho kimehudhuriwa na Waziri wa Katiba na Sheria Mh. George Simbachawene, Katibu mkuu wa wizara hiyo Bi.Marry Makondo, Mkurugenzi wa Haki za Binadamu Bi. Nkasory Sarakikya, pamoja na wajumbe wengine wa wizara hiyo.


Akizungumza kwa niaba ya ujumbe huo, mratibu wa kitaifa wa mtandao wa watetezi wa haki za binadamu Tanzania (THRDC), Onesmo Olengurumwa amempongeza Waziri Simbachawene kwa kuteuliwa kushika nafasi hiyo adhimu, huku  akiutambulisha mtandao na kutoa baadhi ya mapendekezo ya mtandao huo katika kuboresha mashirikiano baina yake na serikali kupitia wizara hiyo.


"Tuna wanachama zaidi ya 200 waliogawanyika katika kanda 11 nchini ambao hufanya Kazi katika maeneo yote ya haki za binadamu, ikiwemo maeneo ya wanawake, pamoja na watoto ambapo wanachama wetu wamekuwa wakishirikiana na wizara ya katiba na sheria pamoja na wizara ya jinsia na watoto, maeneo ya elimu, afya, amani, pamoja na utoaji wa msaada wa kisheria." Olengurumwa


Olengurumwa ameongeza kwa kueleza kazi za mtandao ambapo umekuwa ukifanya Kazi kwa mashirikiano na wizara pamoja na Taasisi zingine za kiserikali ikiwemo, Tume ya Haki za binadamu na utawala bora, Mahakama, bara na visiwani, TAKUKURU, TRA, Pamoja na Ofisi ya Msajili wa mashirika yasiyo ya kiserikali.


Hata hivyo Olengurumwa ameeleza kuwa baadhi ya maeneo muhimu ambayo AZAKI zimekua na mchango wa moja kwa moja kwa Serikali ni pamoja na eneo la utoaji wa huduma za afya, usafi wa mazingira, maji, ambapo kulingana na uchambuzi uliofanywa na serikali katika Mpango wa Maendeleo wa Taifa (FYDP III), AZAKi zimekuwa zikichangia 40% ya uwekezaji katika sekta ya afya. 


Katika majadiliano na wizara, THRDC imefanikiwa kutaja baadhi ya maeneo ambayo yanaweza kufanyiwa maboresho na wizara ikiwemo; 


a) Wizara Kuwa na utataratibu mzuri wa kufahamu, kuripoti na kutambua Kazi zinazofanywa na Watetezi wa Haki za Binadamu kama Wadau muhimu wa wizara hiyo.


b) Kufanyika kwa maboresho katika maeneo ya utoaji wa msaada wa kisheria nchini.


c) Uboreshwaji wa mifumo ya utoaji Haki nchini.


d) Maboresho ya baadhi ya sheria ikiwemo sheria ya NGO, hasa katika upatikaji wa vibali vya tafiti ambavyo huyalazimu mashirika kupitia TAMISEMI Ili kupata vibali hivyo pamoja na sheria zingine.


e) Ushiriki wa wizara katika mikutano na majukwaa ya kimataifa.


f) Tanzania kurudi katika mahakama ya Afrika mashariki.


Pamoja na meneo hayo, THRDC imefanikiwa kutoa mapendekezo ya kufanyiwa Kazi na Wizara katika kuboresha shughuli za utetezi wa Haki za Binadamu nchini. Mapendekezo hayo ni Pamoja na; 


1)  kuboreshwa kwa mfumo wa utekelezaji (Human Rights Enforcement Mechanism - BRADEA) Sheria iliyokuwa inaweka utaratibu wa kulinda  Haki za kikatiba.


Olengurumwa ameeleza kuwa mabadiliko yaliyofanyika yameweka vikwazo/ vingi kwa mtanzania mmoja mmoja au taasisi zao kutekeleza agizo  la ibara ya 26/2 ya kulinda katiba. 


"Kumekuwa na vigingi vingi ambavyo tunaweza kufanya majadiliano na  maboresho kupitia wizara hii ambavyo  yatatoa fursa kwa watanzania naTaasisi za Haki za Binadamu kwenda Moja kwa Moja katika mahakama hii kwa lengo la kulinda na kutetea Haki za Binadamu kupitia mlango wa kikatiba"Olengurumwa


2) Kuwepo kwa National human rights Action plan (Mpango kazi wa Taifa wa haki za Binadamu).


"Serikali iangalie namna ya  kuharakisha kukamilika kwa  mchakato huo Ili Kuwa na andiko litakalotoa mwongozo utawaunganisha wadau wa haki za binadamu na serikali." Olengurumwa


3) Kuwepo na Sera ya Haki za Binadamu ambayo inaweza kutoa mwongozo kwa taasisi binafsi na serikali kuhusiana na Maswala ya Haki za binadamu. 


Sera hii itawatambua na kiwalinda Watetezi wa Haki za Binadamu. Hii ni kuwawezesha wadau pamoja na serikali kuwa na uelewa wa pamoja wa maswala ya utetezi na watetezi wa haki za binadamu nchini. 


4) Eneo la utekelezaji wa Hukumu/maamuzi ya Mahakama za ndani na za kimataifa. 


"Kumekuwa na changamoto za utekelezaji wa maamuzi wa mahakama hasa katika maeneo ya upatikanaji haki 'access to justice'  katika kesi za Haki za Binadamu, lazima uje Dar es Salaam. Tunapendekeza serikali iruhusu kila mahakama yenye hadhi ya mahakama kuu iwe na uwezo wa kusikiliza kesi hizo katika mikoa kesi hizo ziliporipotiwa." Olengurumwa


Baada ya Wasilisho hilo Wawakilishi kutoka Wizara ya Katiba na Sheria walipata wasaha wa kujibu baadhi ya hoja zilizotolewa na THRDC.


Akijibu hoja ya kuwepo kwa Mpango kazi wa Haki za Binadamu (Human Rights Action Plan), mkurugenzi wa Haki za Binadamu kutoka wizara ya Katiba na Sheria, Bi Nkasory Sarakikya ameeleza kuwa wizara hiyo inatarajia kutoa Andiko hivi karibuni, huku akitaja changamoto kadhaa zilizochangia  kuchelewa kwake ikiwemo mchakato wa UPR, lakini kwa kushirikiana na wadau wizara inatarajia kuhakikisha Andiko Hilo linazinduliwa hivi karibuni.


Bi Nkasory amefanikiwa pia kujibu hoja iiliyohoji Mikataba ya Haki za Binadamu iliyoridhiwa na Tanzania, na kueleza kuwa Bado  Kuna taarifa za nchi ambazo Tanzania inatakiwa kuwasilisha, ambapo wizara imeendelea kufanyia kazi maandiko kadhaa ikiwemo CRC na SIDO ambayo yanaandaliwa na wizara za maendeleo ya Jamii, jinsia na watu wenye ulemavu kwakuwa walishaandaa rasimu zao,  hivyo wizara ya Katiba na sheria inatarajia kufanya uhakiki na kukamilisha michakato kwa ajili ya kuwasilishwa kwake. Maandiko ya ACCPR Pamoja na Maputo Protocol yote yatawasilishwa hivi karibuni.


"Tukiwa tunaandaa taarifa za nchi, mara zote serikali imekuwa ikiwahusisha wadau wa Haki za Binadamu ikiwemo CSO's zote Tanzania bara na visiwani. Hii inatusaidia sana kujua nini kinaendelea Nchini kwani nyinyi mna reach kubwa sana  mnatusaidia kufika kule tusipoweza kufika msaada wenu unakuwa mkubwa sana kwetu"  Nkasory Sarakikya


Katika swala la utolewaji elimu kwa wasaidizi wa kisheria, wizara imeeleza kuwa inaona umuhimu mkubwa na ipo tayari kushirikiana ma wadau kutoa elimu kwa wasaidizi wa kisheria ambao wamekuwa msaada mkubwa katika kutatua baadhi ya changamoto nyingi zinazoikumba jamii  ikiwemo maswala ya  usuluhishi na kupunguza wingi wa mashauri mahakamani, hivyo wizara ipo tayari kushirikiana na Watetezi wa Haki za Binadamu kukamilisha Hilo.


Baada ya majibu ya hoja hizo kutoka kwa watumishi wa wizara, waziri Simbachawene ameelezwa kufurahishwa na ujumbe uliomtembelea ambao umezingatia usawa wa kijinsia pamoja na kujumuisha Wadau kutoka pande zote za muungano.  Lakini pia Waziri Simbachawene

ameipongeza hatua iliyochukuliwa na wadau wa sekta ya AZAKI katika kuona umuhimu wa kukutana na wizara na kuwasilisha mapendekezo hayo kwa malengo ya mashirikiano huku akiwakaribisha wadau wengine kujtembelea wizara hiyo kwa malengo ya mashirikiano.


Waziri Simbachawene ameelezwa kuwa 


"Tanzania ni nchi ambayo inatambua, inaheshimu, inatunza  na kulinda Haki za binadamu, hivyo sisi tunashirikiana na ninyi taasisi hizi za wadau na wa Haki za Binadamu na katika kazi nyingi mnazozifanya kweli zinasaidia Serikali." Waziri Simbachawene


Ameongeza kuwa  katika mwaka mmoja wa uongozi wake,  Rais Samia amedhihirisha nia ya kutanzua maeneo ambayo yameonyesha kuwa na shida katika eneo la Haki za Binadamu na amekuwa akifanya hivyo kwa vitendo, na nadharia, huku akiahidi mashirikiano zaidi ya wizara yake na wadau wa Haki za binadamu nchini.


"Wizara ya Katiba na sheria imefurahi kuona mpo na itaendelea kushirikiana na nanyi katika kila jambo ambalo mtapenda tushirikiane." Waziri Simbachawene


Waziri Simbachawene amewataka watetezi wa Haki za Binadamu nchini kuhoji na kuzungumza na wizara pale kunapotokea jambo lenye ukakasi katika serikali, badala ya kupeleka hoja katika majukwaa ya kimataifa  na kuiondolea heshma nchi.  Ameeleza kuwa Nchi ya  Tanzania ndio mama yetu hivyo inapaswa kujengwa kwa ushirikiano.


Ameongeza Kuwa wizara ya katiba na sheria itakuwa ya mwisho kuchoshwa na taasisi yoyote katika nchi ambayo itakiuka maadili ambapo kazi kubwa ya wizara itakuwa ni kuirudisha taasisi hiyo kwenye mstari.


Hata hivyo waziri Simbachawene ameongeza Kuwa wizara itashiriki kwa pamoja na wadau wa AZAKI katika majukwaa ya kimataifa Ili kuhakikisha Tanzania inajengwa kwa mashirikiano thabiti na yenye tija kati ya AZAKI na Serikali.


Akijibu hoja ya Tanzania kujitoa katika mahakama ya Afrika, Waziri Simbachawene ameeleza kuwa, katika swala hilo zilikuwepo na sababu, lakini haziwezi kuwa za Kudumu, hivyo mazungumzo yanaendelea ndani ya Serikali na anaamini Tanzania itarudi tena katika Mahakama hiyo.


"Mahakama hii ipo Tanzania, inakuwa si vizuri sana kama tena sisi watanzania kutokuwa kule. Tupewe muda, mchakato unaendelea nina imani si muda mrefu maamuzi yatatolewa na serikali" Waziri Simbachawene


Mwisho Waziri Simbachawene ametoa maelekezo kwa wizara kuona mamna itaboresha mfumo wa kushughulikia maswala ya Haki za Binadamu, hasa kwa wizara kushirikiana na Wadau wa Haki za Binadamu kupitia tafiti zilizofanyika,   Ili kuweka mfumo mzuri wa uboreshwaji wa Haki za Binadamu, hasa katika maswala ya ufunguaji kesi zenye maslahi kwa umma.


Mwisho Mratibu amemkaribisha Waziri katika maadhimisho ya miaka 10 ya mtandao yanayotarajia kufanyika mwezi Aprili mwaka huu ambayo kwa kiasi kikubwa yanatarajia kuungwa mkono na wizara hiyo katika mambo kadha wa kadha.


Hatua hii ni mwendelezo wa jitahada za mtandao wa THRDC kuendelea kushirikiana na serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania kupitia  wizara, taasisi, na wadau mbali mbali katika kuhakikisha Watetezi wa Haki za Binadamu nchini wanapata fursa ya kufanya Kazi kwa ukaribu na serikali katika kuweka mikakati ya pamoja yenye malengo ya kuisaidia jamii ya 

Share To:

Adery Masta

Post A Comment: