Na Ahmed Mahmoud Taasisi ya Utafiti Tari Selian imekusanya sampuli za udongo katika mikoa 14 ya Tanzania bara ili kubaini kiasi cha mbolea kinachohitajika kukuzia mazao ikiwemo maharagwe aina ya Jesca. Aidha Tanzania imepitisha aina mbili za mbegu bora za maharagwe zenye madini ya.chuma na zinki ambazo ni selian14/na selian15 lengo likiwa ni kupunguza utapiamlo nchini na ukanda wa Afrika mashariki. Hayo yamesemwa na Kaimu Mkurugenzi wa taasisi hiyo Dkt.Emmanuel Mgonja wakati wa ziara ya waandishi wa habari katika Kituo hicho waliokuwa kwenye mafunzo ya habari za Sayansi Teknolojia na ubunifu yaliyoandaliwa na Costech. Alieleza kwamba tokea kuanzishwa kwake kituo kimeweza kugundua kuendeleza tafiti na kuzalisha takribani aina 50 za mbegu ikiwemo maharagwe15 mahindi 12 mbaazi 6 ngano 11 na shayiri 6. Alibainisha kwamba mafanikio ya kituo hicho ni kuwa na ushirikiano mkubwa na makampuni ya mbegu wenye lengo la kuongeza kasi ya uzalishaji wa mbegu bora utakaosaidia kuongeza mazao yenye ubora unaokubalika kwenye masoko ya kimataifa. Akiongelea dhima ya taasisi ni kugundua na kuhimiza teknolojia mbalimbali za kilimo ili kuongeza tija na uhakika wa chakula na lishe kwa kilimo endelevu chenye mchango chanya katika ukuaji wa uchumi wa nchi. "Hapa selian kituo kimeweza kuongeza thamani ya mazao hususani maharagwe mbaazi na ngano, kupitia teknoljia ya habari na mawasiliano kwa kutumia simu janja kushauri matumizi sahihi ya mbolea kwa maafisa ugani katika wilaya za Arumeru Moshi vijijini na Siha." Awali akiongea katika mafunzo hayo Mtafiti Msaidizi Tari Selian Mosses Bayinga Alisema kituo hicho kimejikita katika utafiti na kuendeleza zao la shayiri Ngano Maharagwe Mahindi pia uzalishaji wa rasilimali asili udongo miti na majani. Kwa Upande wake Mratibu wa mafunzo hayo kutoka Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia COSTECH Deusdedit Leonard amesema kuwa mafunzo hayo kwa wanahabari yamelenga kuchakata lugha ngumu ya kiutafiti inayotolewa na watafiti ili kuweza kueleweka kwa jamii na kuleta matokeo chanya. Alisema kwamba taasisi hiyo ndio imekuwa ikiratibu shughuli zote za kisayansi teknolojia na ubunifu hapa nchini ambapo wao ndio washauri wakuu wa serikali kuhusiana na teknolojia ubunifu na sayansi. "Sisi ndio tunazisimamia taasisi za maendeleo na ubunifu kama Tari Temdo Camartec n.k.ndio wadau wetu pia vyuo vya elimu ya juu wao hufanya Utafiti ili kuwafikia walengwa ndio hapo wanaingia wanahabari ili matokeo ya sayansi yawafikie wananchi kwa njia rahisi"
Share To:

Arusha Newsroom

Post A Comment: