Mratibu wa Taasisi ya Sisi Tanzania Mkoa wa Singida Shabani Mukee (katikati) akizungumza wakati akiongoza kikao cha viongozi wa taasisi hiyo kilichofanyika leo mjini hapa abapo walimpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutimiza mwaka mmoja madarakani.
Mratibu wa Taasisi ya Sisi Tanzania Mkoa wa Singida Shabani Mukee akiongoza kikao hicho.
Viongozi wa taasisi hiyo wakiwa meza kuu. Kutoka kushoto ni Katibu Mkuu wa Taasisi hiyo, Mwalimu Tumaini Kalikule, Mratibu wa Taasisi hiyo Mkoa wa Singida, Shabani Mukeena Mratibu Msaidizi wa Taasisi hiyo Mkoa wa Singida Yahaya Njiku.
 Mratibu wa Taasisi hiyo Mkoa wa Singida, Shabani Mukeena Mratibu Msaidizi wa Taasisi hiyo Mkoa wa Singida Yahaya Njiku akizungumza katika kikao hicho na kutoa pongezi kwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutimiza mwaka mmoja tangu awe Rais wa Tanzania.
Kikao kikiendelea.
Kikao kikiendelea.
Kikao kikiendelea.
Mshiriki wa kikao hicho Paschal Masele akichangia jambo kwenye kikao hicho.
Meneja Mradi wa Taasisi hiyo, Rebecca Wellia akichangia jambo.
Katibu wa Taasisi hiyo Wilaya ya Itigi, Charles Chimala akichangia jambo.
Mweka Hazina wa Taasisi hiyo, Omary Hamisi akizungumzia umuhimu wa vijana kuilina amani ya nchi yetu.
Mmoja wa washiriki kutoka Wilaya ya Ikungi akichangia jambo kwenye kikao hicho.
Picha ya pamoja.


 

Na Dotto Mwaibale, Singida

 

TAASISI ya Sisi Tanzania Mkoa wa Singida imempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutimiza Mwaka Mmoja wa Uongozi wake tangu alipoingia madarakani. 

Akizungumza wakati wa kutoa pongezi hizo katika kikao cha viongozi wa Taasisi hiyo kilicho keti leo Ukumbi wa Kanisa la Romani Katoliki (Social) mjini hapa , Mratibu Msaidizi wa Taasisi hiyo Mkoa wa Singida Yahaya Njiku alisema Watanzania wanakila sababu ya kumpongeza Rais Samoa Suluhu kutokana na uongozi wake uliotukuka. 

"Katika kipindi cha mwaka mmoja tangu awe madarakani Rais Samia Suluhu Hassan ameonesha uwezo mkubwa wa kuongoza nchi kwani amefanya mambo mengi ambayo Watanzania hawakuyategemea" alisema Njiku. 

Alisema Taasisi hiyo itaendelea kuunga mkono jitihada zake zote za kuongoza nchi na kuwaletea maendeleo Wananchi wa Tanzania. 

Wakati huohuo Mweka Hazina wa  Taasisi hiyo Omary Hamisi amewataka vijana mkoani hapa  kuendeleza kudumisha amani na utulivu wa nchi ambao tumeachiwa na waasisi wa taifa letu Hayati Julius Kambarage Nyerere na wenzake.

"Vijana ni kundi kubwa ambalo linatakiwa kwa nguvu moja kuitunza amani na utulivu wa nchi yetu hivyo tuna kila sababu ya kufanya hivyo" alisema.

Alisema Taasisi hiyo malengo yake makubwa ni kuisaidia serikali katika shughuli mbalimbali za maendeleo  na kutekeleza mambo mbalimbali yanayowagusa vijana.

Mratibu wa Taasisi hiyo Mkoa wa Singida Shabani Mukee alisema kikao hicho kiliketi kwa ajili ya kujadili ajenda kadhaa ikiwemo ya kuandaa kongamano la uzinduzi wa taasisi hiyo, kuwa na sare za taasisi na kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutimiza mwaka mmoja wa kuwa madarakani ambapo amefanya kazi kubwa katika sekta mbalimbali kwa ajili ya kuwaletea maendeleo wananchi.

Mukee alitaja mambo mengine yaliyojiri kwenye kikao hicho kuwa ni ufunguzi wa kikao, utambulisho, kutoa taarifa ya utambulisho wa taasisi hiyo kutoka kwa mkuu wa mkoa na  taasisi kuwa na ofisi ya mkoa.

Kikao hicho kilihudhuriwa na viongozi wote kutoka wilaya zote za Singida ambazo ni Iramba, Itigi, Mkalama, Manyoni, Ikungi, Singida Mjini na Singida DC.


Share To:

dotto mwaibale

Post A Comment: