Na,Jusline Marco:Arusha

Kamati ya siasa Mkoa wa Arusha imetembelea na kukagua miradi mbalimbali katika sekta  ya elimu, afya  pamoja na miundombinu ya Barabara katika Wilaya ya Aruneru na kuridhishwa na kazi iliyofanyika.


Mjumbe wa kamati ya siasa Mkoa wa Arusha Bw. Moloiment  Olemoko akiwa mgeni rasmi katika ziara hiyo amesema kuwa utekelezaji wa miradi hiyo imezingatia ila Ilani ya Chama cha Mapinduzi pamoja na maelezo yanayotolewa na serikali ya awamu ya sita iliyopo chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassani.


Bw .Olemoko ametembelea mradi wa ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa  katika shule ya msingi Enaboishu Academy yenye mchepuo wa kingereza,mradi ulio gharimu shilingi million 20 na laki 4,lakini pia ametembelea mradi wa ujenzi wa  kituo cha afya  cha Olorien uliogharimu shilingi million 450 hadi kukamika kwake.


Kamati ya siasa ya Mkoa ilipofika katika shule ya msingi Enaboishu Academy kukagua ujenzi wa madarasa .

Olemoko amesema kamati hiyo amefurahishwa na  ukamilikaji wa miradi hiyo kwa wakati  na kwa kuzingatia bajeti iliyotengwa na serikali ambapo  fedha hizo zimetokana na mapato ya ndani ya halmashauri  yanayotokana na kodi za wananchi.


Aidha amesema licha ya miradi hiyo kukamilika ,bado mradi wa kituo cha afya cha Mwandeti haujakamilika kutokana na changamoto  mbalimbali ikiwemo ubovu wa miundombinu ya barabara na ukosefu wa maji ambapo wameiomba serikali kuwatatulia changamoto hiyo.


Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhandisi Richard Ruyango katika ziara hiyo amesema  juhudi za serikali  ya awamu ya sita  ni kupanua wigo wa vyumba vya madarasa  pamoja na kuongeza vituo vya afya katika wilaya hiyo.


Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhandisi Richard Ruyango akizungumza katika ziara ya kamati ya siasa ya Mkoa iliyotembelea miradi inayotekelezwa na serikali ya awamu ya sita.

Katika hatua nyingine Mhandisi Ruyango amewaomba waalimu kuwa wabunifu katika kuwafundisha watoto kwa bidii kwa kuwa  taifa linapambana na ujinga, umaskini na maradhi hivyo wanapaswa kuwapatia watoto elimu bora itakayo likomboa taifa  hapo baadae na kuwaomba wananchi kutunza miundombinu hiyo ili iweze kutumiwa na vizazi vijavyo.


Amesema  kuwa  serikali  ya awamu hiii imewekeza fedha nyingi katika idara ya Elimu ambapo katika Wilaya ya Arumeru imetoa fedha za kujenga madarasa 170 ambapo amesema kuwa kufuatia ilani ya chama cha Mapinduzi CCM serikali imetoa  shilingi bilioni 2.4 za ujenzi wa miundombinu ya barabara katika wilaya  hiyo.



Kwa  upande wake mwalimu  Mkuuu wa shule ya  Sekondari Kimyanki Paschal Ginana ameishukuru serikali  kuu kwa kuwekeza nguvu nyingi kwenye sekta ya elimu.

Share To:

JUSLINE

Post A Comment: