Naibu waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Bi Paulne Gekul Machi 21. 2022 Jijini Dodoma amewapongeza wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi kwa kuchaguliwa na kuaminiwa kuwa wanaweza kusimama mbele na kuwawakilisha wenzao katika mkutano huu wakitoka katika idara na vitengo vyao.

“Tunatambua kuwa kila mtumishi wa wizara hii anafanya kazi kwa juhudi kubwa na mambo mengi sana ambayo yanaonekana kwa macho, naomba nitumie fursa hii kuwapongezeni kwa juhudi zenu hizo.”

Naibu Waziri Gekul aliongeza kuwa yeye jukumu lake ni kumsaidia Waziri Mchengerwa kwa kuyafanikisha malengo ya serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mheshimiwa Samia Suluhu Hassan na taifa letu linasonga mbele.
Share To:

Post A Comment: