Na Mwandishi Wetu.

 

Mtandao unaoongoza katika utoaji wa huduma za Kidigitali hapa nchini Tigo Tanzania kwa mara nyingine tena umedhamini Mashindano ya Mbio za Riadha Kilomita 21 ikiwa ni mara ya saba mfululizo  maarufu kama TIGO KILI HALF MARATHON yatakayofanyika tarehe 27 Februari katika viwanja vya Ushirika mjini Moshi. Akizungumza katika uzinduzi wa Mbio hizo Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Kaskazini Bw. Henry Kinabo amesema kuwa


                                           

 'Nipende kuchukua fursa hii kuwakaribisha wote  katika hafla hii ya uzinduzi wa mbio za Kilimanjaro Marathon 2022 zitakazo fanyika hapa mkoani Kilimanjaro, Mjini Moshi ambako ni mojawapo wa kitovu kikubwa cha shughuli za kiuchumi ikiwemo utalii.Ningependa kuchukua fursa hii kuwapongeza waandaji wa Kilimanjaro marathon,kwa kufikisha miaka 20 ya kuandaa,kuratibu mbio hizi za kimataifa,  Kampuni ya Tigo imeendelea kuwa mstari wa mbele katika kuhamasisha utalii kwa kutumia njia mbalimbali ikiwemo kudhamini mbio za nusu marathoni maarufu kama Tigo Kili Half Marathon (21). Mwaka huu, Tigo imedhamini tena mbio hizi maarufu za Tigo Kili Half Marathon (Km 21) ikiwa ni mara ya saba mfululizo, ili kutoa fursa kwa watanzania na watu kutoka nchi jirani kushiriki, kubadilishana tamaduni,kuburudika na kufurahi kwa pamoja.

 


Mwaka jana tulizindua mradi wetu wa Tigo Green for Kili,ulio kuwa na dhamira ya kuboresha mazingira na kurudisha theluji katika Mlima Kilimanjaro,mradi huu endelevu ukiwa na lengo la kupanda miche 28,000. Mwaka huu tumejipanga kufanya mengi zaidi kwaajili ya mradi huu kwani muamko ulikuwa mkubwa sana kutoka kwa makampuni na wadau mbali mbali.' Alimalizia Bwana Kinabo

Kumbuka Dirisha la usajili kwaajili ya Tigo Kili Half Marathon 2022 pamoja na mbio za Km 42 na Km5 limekwisha kufunguliwa na wateja wa Tigo wanaweza kupiga *149*20# ili kujisajili na kufanya malipo.

Ili kujisajili,mteja wa Tigo atatakiwa kupiga *149*20# kisha kuchagua aina ya mbio anazotaka kushiriki na kufuata maelekezo kwaajili ya kufanya malipo na baadaye atapokea ujumbe wa kuthibitisha malipo yake.

Mshiriki wa mbio hizi anatakiwa kuhifadhi ujumbe (SMS) na atatumia kama uthibitisho akiambatanisha na kitambulisho chake wakati wa kuchukua namba ya ushiriki katika vituo vilivyopo Dar es Salaam, Arusha na Moshi.

Katika mbio hizi, Tigo inatoa zawadi za kifedha zenye thamani ya Shilingi Milioni 12.5 kwa washindi 10 wa kwanza wa Tigo Kili Half Marathon (wanawake na wanaume).Pia,washiriki 4,500 watakaomaliza Km 21 watapewa medali za heshima.Vilevile, tutatoa vyeti  kwa washiriki wote wa Tigo Kili Half Marathon.

Lakini pia wateja wa Tigo wataweza kuwatumia marafiki, ndugu na jamaa, matukio mbali mbali matukio yatakayokuwa yanaendelea siku hio kupitia mtandao wetu ulioboreshwa  kupitia mitandao ya kijamii kwa kutuma picha na video kupitia intaneti ya kasi ya 4G.






Share To:

Adery Masta

Post A Comment: