Naipongeza Kamati Kuu ya CCM chini ya Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa kumteua Dr Tulia Ackson Mwansasu kuwa mgombea nafasi ya Uspika katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi. 

Ana sifa, uwezo, uzoefu na amedhihirisha uwezo wa kumudu changamoto za kuliongoza Bunge kwa weledi, umahiri na ufanisi. Wana CCM na Watanzania wote hatuna budi kuungana na Kamati Kuu ya CCM kwenye uteuzi huu ili kuhakikisha Bunge letu linapata Spika atakayeweza kusimamia utekelezaji kikamilifu wa  majukumu ya Bunge na kuishauri Serikali jinsi ya kukabiliana na changamoto za sasa hivi. William Sarakikya MNEC Taifa Viti 15 Bara.

Share To:

Post A Comment: