Mh Neema Lugangira akiwa katika moja ya vikao vyake na Wavuvi wa Bukoba Manispaa mwaka 2020
Mwenyekiti wa Chama Cha Wavuvi Mkoa wa Kagera  Ndg. Merdad Kaijage akizungumza wakati wa mkutano huo
Katibu Alex Bakenjela akizungumza wakati wa mkutano huo

Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera, Prof Kamuzora akizungumza wakati wa mkutano huo
Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera, Prof Kamuzora akizungumza wakati wa mkutano huo


NA MWANDISHI WETU, KAGERA

 

CHAMA cha Wavuvi Mkoani Kagera kimemchagua Mbunge wa Viti Maalumu kupitia Kundi la Asasi za Kiraia Tanzania Bara (NGOs) Neema Lugangira kuwa mlezi wa chama hicho wakati wa mkutano mkuu wao uliofanyika Januari 20 mwaka huu.

 

Akitangaza uamuzi huo leo wakati wa mkutano mkuu chama hicho uliofanyika katika Ukumbi wa Linas uliopo Manispaa ya Bukoba ambapo Mwenyekiti wa chama hicho Merdard Kaijage alisema chama wameazimia kwa pamoja kumpitisha Mbunge Neema Lugangira kuwa mlezi wao.

 

Alisema chama hicho kinahitaji walezi ambao watawasaidia kuendeleza chama na kuwasemea wavuvi huku akieleza mlezi huyo ni mtu sahihi kwao kuweza kuwa chachu kubwa ya maendeleo kutokana na mchango mkubwa ambao amekuwa akiutoa kwa jamii.

 

Mkutano huo mkuu ulihudhuriwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera, Prof Kamuzora ambaye alikuwa mgeni Rasmi wa Mkutano wa Chama Cha Wavuvi Mkoa Kagera,Mwenyekiti wa Chama Cha Wavuvi, Ndg. Merdad Kaijage, Katibu Alex Bakenjela, Afisa Ushirika wa Mkoa wa Kagera na Wavuvi ambao ni Wanachama. 

 

Katika Mkutano huu chama hicho kilitumia nafasi hiyo kujadili na Kupitisha Katiba ya Chama n ambayo itakuwa ni silaha kubwa ya kuweza kuendesha masuala mbalimbali kisheria

 

Akizungumza wakati akifungua mkutano huo Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera ( RAS) Prof Kamuzora alisema siku zote wavuvi wanafanya kazi zao kwa kujitenga, hawakuwa na chombo cha kuwaunganisha na Kuwasemea hivyo hatua hii ya kuwa na Chama Cha Wavuvi Kagera kitasaidia sana kujenga na kuinua Sekta ya Uvuvi Mkoa wa Kagera. 

 

Alisema Mkoa wa Kagera una fursa nyingi lakini hazitumiki ipasavyo kuinua Uchumi wa Kagera hivyo aliahidi kutoa Ushirikiano wa kila hali utakapohitajika. 

 

Prof Kamuzora aliwataka wavuvi wawe wamoja kuanzia Wavuvi Ziwani, Wafugaji wa Samaki pamoja na wanaojishughulisha na Uvuvi Ziwa Burigi huku akitoa wito kwao kuacha kushiriki kwenye vitendo vya uvuvi haramu.

 

Kwa upande wake Katibu wa Chama Cha Wavuvi Kagera, Ndg. Alex Bakenjela alimuhakikisha Katibu Tawala huyo kuwa chama hiki hakitashirikiana na Mwanachama yeyote atakaejihusisha na Uvuvi Haramu na watakuwa tayari kuwafichua watakaobainika kushiriki kwenye vitendo vya namna hiyo 

 

Wajumbe wa Chama cha Wavuvi Kagera wote kwa pamoja walifunga Mkutano huu kwa Kumpogeza Mhe Rais Samia Suluhu Hassan, Rais wa Tanzania kwa kazi nzuri anayofanya pamoja na Wasaidizi Wake. 

 

Share To:

TANGA RAHA BLOG

Post A Comment: