Joel Maduka Geita
Mbunge wa jimbo la Msalala Idd Kassim Idd amekerwa na kusikitishwa na kitendo cha wakala wa barabara mjini na vijijini ( Tarura) halmshauri ya msalala Wilayani Kahama , Kwa kitendo kuwapa tenda wazabuni wasio kidhi vigezo na kusababisha barabara kurudiwa pamoja na kutokukamilika kwa wakati
Mbunge Idd amesema hayo leo january 10, 2021 pindi alipokutana na maafisa wa Tarura katika kijiji cha Bubungu kata ya Jana ambapo amewata tarura wawe wanatoa taarifa za miradi inayotekelezwa ndani ya. jimbo lake ili kuwaondolea hofu na kuwambia wananchi namna serikali yao inavyopambana kuwarekebishia miundo mbinu kijiji kwa kijiji ,kata kwa kata nchi nzima .
" Tarura mnasema mmepokea fedha za tozo kwa ajili ya barabara lakini amtoi taarifa kwenye ofisi yangu Kama msimamizi wa Jimbo ni lazima mimi nijue mnatekeleza barabara gani , gharama gani ,na fedha kutoka wapi ili tuwaeleze wananchi sio mpaka tufumaniane site"
Mbunge Idd amechangia kiasi cha shillingi million 2. ili kukamilisha ujenzi wa msingi wa hosteli ya shule ya Sekondari ya Kata ya jana itakayowasaidia wanafunzi kukaa na kupata muda mwingi wa kujisomea sambamba na kuepukana na vishawishi vibaya vitakavyoharibu ndoto zao.
Post A Comment: