Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro  ametembelea na kujionea mwitikio wa wanafunzi walioripoti shule hususani darasa la awali na la kwanza pamoja na kidato cha kwanza ambao wameanza kuhudhuria masomo yao Januari 17 mwaka huu katika Mji  mdogo wa Loliondo na kuridhishwa na mwitikio huo.


Mwangwala amesema kuwa tayari Serikali imejenga madarasa ya kutosha kwa ajili ya watoto wote wa kidato cha kwanza na kuongeza kuwa hakuna mtoto atakayebaki nyumbani kwa kisingizio cha kukosa sare au mahitaji na kutoa madaftari, kalamu na sare kwa watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu.

Share To:

Post A Comment: