Wednesday, 22 December 2021

Waziri Ummy atoa siku saba kwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Singida kukamilisha jengo la X-ray Kituo cha Afya Sokoine

 


Nteghenjwa Hosseah, OR-TAMISEMI


WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa, na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) Ummy Mwalimu ametoa siku saba kwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Singida kuhakikisha anapeleka Sh.26 Milioni kwa ajili ya kukamilisha  ujenzi wa jengo la X-Ray katika Hospitali ya Sokoine ili kuwaondolea adha wananchi wanaokosa huduma hiyo.


Hatua hiyo imefikiwa jana na Waziri Ummy baada ya kupokea taarifa ya ujenzi wa jengo hilo na kubaini kusuasua wakati akiwa katika ziara ya kikazi ya siku moja katika Manispaa hiyo ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo.


"Mkurugenzi nakupa wiki moja leta Sh. Mil. 26 hapa kwa sababu mapato mnayo nahitaji jengo la X-ray likamilike waoneeni huruma watu wa singida" alisema Ummy.


Alisema jambo la kushangaza ni pale Mkurugenzi anapooneka kutokuguswa na mradi huo na kutoona unuhinu wa kupeleka fedha za ukamilishaji na akahoji kwanini fedha hizo zinatolewa kidogo kidogo kama fedha za hisani wakati ni fedha za wananchi? 


‘Nimefurahishwa  na mradi huu  kwa kuwa unatekelezwa kwa fedha za mapato ya ndani lakini haiwezekani ujengwe kwa miaka mitatu mradi unatakiwa ujengwe kwa mwaka mmoja na kama ikishindikana isizidi miaka miwili ili muendelee  na jambo jingine’ alisema Ummy


‘Aliongeza kuwa fedha hizo si hisani zinatolewa na wananchi wa Singida kutokana na ushuru mbalimbali wanaolipa hivyo wanapaswa kuzirudisha kwao ili zikatatue kero zao za maendeleo’ 


"Mkuu wa wilaya nakuachia jambo ili ulisimamie leo ni tarehe 21 nataka mpaka tarehe 31 Desemba fedha hizo ziwe zimekwisha letwa hapa hakuna cha sikukuu fedha hizo ziwezimefika" alisisita Mwalimu.


Akisisitiza umuhinu wa uwepo wa Jengi hilo katika Kituo cha Afya Sokoine Mkurugenziw a Afya Ustawi wa Jamii na Lishe toka OR-TAMISEMI Dkt. Ntuli Kapologwe amesema idadi wa wanawake wanaojifungua katika kituo cha Afya Sokoine ni 400-600 kwa mwezi hivyo muhimu sana kuwepo wa jengo la X-ray ili kutoa huduma wakati wa ujauzito wao.

No comments:

Post a Comment