Vijana wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) wang'arisha Taasisi hiyo kwa kupanda Mlima Kilimanjaro.

 KATIKA kuelekea Maadhimisho ya Miaka 60 ya Uhuru, Wanachuo kutoka Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) wamevunja rekodi ya kupanda Mlima kilimanjaro kwa siku 3 tu badala ya siku 6 kama ambavyo imezoeleka kwa watu wengine wanaopanda mlima huo.

Wanachuo hao wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania  Innocent George Masanja anayesoma Shahada ya Uongozi wa Rasilimali watu na Fadhili Jonathan Naaman anayesoma Shahada ya Usimamizi wa Biashara wamepanda Mlima Kilimanjaro mapema wiki hii.

Tukio hili la kihistoria limeipeperusha bendera ya Taasisi ya Uhasibu (TIA) kitaifa na kimataifa, na hakika TIA inajivunia kuwa na vijana Shupavu, Jasiri na wachapakazi.

Taasisi ya Uhasibu Tanzania itaendelea kutoa elimu yenye ufanisi inayomjenga Mwanachuo kujitegemea na kujiamini ili kuhakikisha anatimiza malengo yake.
Share To:

Post A Comment: