Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akizungumza wakati wa ufunguzi wa kikao na Mawakala Binafsi wa Huduma za Ajira nchini, uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam.

Mwakilishi wa Mawakala Binafsi wa Ajira ambaye pia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya JMaselle Investiment Bw.Jeremiah Maselle akizungumza wakati wa ufunguzi wa kikao na Mawakala Binafsi wa Huduma za Ajira nchini, uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam. Aliyefungua kikao hicho ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama.

Mawakala Binafsi wa Ajira wakiwa katika ufunguzi wa kikao na Mawakala Binafsi wa Huduma za Ajira nchini, uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam. Aliyefungua kikao hicho ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama. Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akipata picha ya pamoja na baadhi ya Mawakala Binafsi wa Ajira katika ufunguzi wa kikao na Mawakala Binafsi wa Huduma za Ajira nchini, uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam. Aliyefungua kikao hicho ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama. Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akipata picha ya pamoja na baadhi ya Mawakala Binafsi wa Ajira katika ufunguzi wa kikao na Mawakala Binafsi wa Huduma za Ajira nchini, uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam. Aliyefungua kikao hicho ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama. Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akipata picha ya pamoja na baadhi ya Mawakala Binafsi wa Ajira katika ufunguzi wa kikao na Mawakala Binafsi wa Huduma za Ajira nchini, uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam. Aliyefungua kikao hicho ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama. Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akipata picha ya pamoja na baadhi ya Mawakala Binafsi wa Ajira katika ufunguzi wa kikao na Mawakala Binafsi wa Huduma za Ajira nchini, uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam. Aliyefungua kikao hicho ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama.

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

*************************

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

Waziri wa nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe.Jenista Mhagama amewataka mawakala wa ajira binafsi kuwapatia vipaumbele vijana waliohitimu masomo ya fani mbalimbali na siyo kupeleka wafanyakazi wa ndani katika masoko ya ajira za nje

Ameyasema hayo leo Jijini Dar es Salaam wakati akifungua Kikao na Mawakala Binafsi wa Huduma za Ajira nchini ili kujadili changamoto mbalimbali ili kuona namna ya kusaidia kupunguza tatizo la ajira.

Amesema katika kusaidia kupunguza tatizo la ajira, Tanzania ina vijana wengi wenye elimu na hawana kazi ila mawakala hao wamekuwa wakikazana kupeleka wafanyakazi wa ndani.

Amesema baadhi ya kampuni hazina leseni za kufanya kazi za Uwakala wa ajira na baada ya kukaguliwa walibaini kuwa nyaraka walizokuwa wakitumia ni batili, siyo halali ili wajipatie leseni za kufanya biashara za uwakala.

“Tatizo kubwa la ajira ni kwa vijana waliosoma, wahitimu wapo wanamaliza kila siku na tukienda katika hizo nchi tunakuta na watu waliosoma kwa viwango tofauti kutoka nchi nyingine wanafanya kazi kwanini sisi hatuhangaiki na hao tunataka tukawakusanye watu Njombe tuwapeleke huko,” Amesema

Aidha ameilekeza Ofisi yake kuhakikisha Makampuni ya Uwakala Binafsi wa Huduma za Ajira watakaoomba usajili na ambao wameshaomba wafanyiwe ukaguzi kabla na baada ya kupata usajili ili kubaini mapungufu ya utekelezaji wa Sheria ya Huduma ya Wakala Binafsi wa Ajira Na.9 ya mwaka 1999 pamoja na Kanuni zake za mwaka 2014.

Amesema wameimarisha usimamizi wa huduma za ajira kwa kuanzisha na kukijengea uwezo Kitengo cha Huduma za Ajira (TaESA) ili kiweze kusimamia na kuratibu ipasavyo utafutaji wa fursa za ajira ndani na nje ya nchi pamoja na michakato ya kuunganisha watanzania na fursa husika.

Pamoja na hayo amesema Serikali itaendelea kuimarisha usimamizi na udhibiti wa shughuli za Wakala wa Ajira ili ziweze kutekeleza shughuli zao kwa weledi na uadilifu na hivyo kuchangia katika kupunguza tatizo la ajira nchini, kukuza uchumi na kuchangia pato la Taifa.

Akizungumza kwa niaba ya mawakala hao,Bw. Jeremiah Maselle ambaye ni Mkurugenzi wa kampuni ya JMaselle Investiment amesema ujio wa waziri eneo hilo utatoa majibu ya matatizo yao ambayo wamekuwa wakiyalalamikia kwa muda mrefu.
Share To:

emmanuel mbatilo

Post A Comment: