Baada ya kumalizika mkutano wa 29 Baraza la Mawaziri wa Maji kutoka nchi wanachama wa Bonde la Mto Nile Novemba 26,2021 Naibu Waziri wa Maji Mhandisi Maryprisca Mahundi(Mb)ametembelea mto Nile.


Mto Nile ndiyo tegemeo kwa ukanda huo mbali ya kusambaza maji majumbani pia hutumika kwenye shughuli za kiuchumi kama kilimo.


Mkutano huo uliofanyika kwa mafanikio makubwa umejumuisha nchi za Uganda,Sudan ya Kusini,Burundi,Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo,Kenya,Sudan na Eliteria.


Pamoja na mafanikio hayo Baraza limepitia bajeti ya fedha kwa mwaka 2021/2022.

Share To:

Post A Comment: