Thursday, 11 November 2021

Wadau wa Afya Wekezeni kwenye Rasilimali Watu’ Mhe Ummy

 ‘


Nteghenjwa Hosseah, Dodoma


Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Ummy Mwalimu amewataka wadau wanaotekeleza Afua za nchini kuwekeza kwenye ajira za  watumishi wa Afya ili kukabiliana na upungufu wa watumishi wa kada hiyo uliopo hivi sasa.


Waziri Ummy ameyasema hayo wakati wa kufunga mradi wa USAID Boresha Afya Kanda ya Kaskazini, Kati na Kusuni iliyofanyika leo Jijini Dodoma.


Amesema nimesikia changamoto mbalimbali zilizowasilishwa na wadau ambao wametekeleza kazi za mradi huu ikiwemo upungufu wa watumishi, hii ni changamoto ambayo Serikali inaitambua na inatoa kipaumbele na mpaka sasa tumeshapeleka maombi ya Kibali cha Ajira Utumishi ili tuweze kuajiri wataalamu hao.


“Watumishi wa Afya waliopo hivi sasa ni 47% tu ya mahitaji hivyo tuna upungufu wa 53% hata tukiajiri hatuwezi kumaliza tatizo hili hivyo ni vyema na wadau wetu mkatuunga mkono” alisema Ummy.


Kila Mdau akiweka kipengele cha kuajiri wataalam wa Afya hata wawili tu kwa mwaka itasaidia katika kuboresha eneo hilo na kwa pamoja tukazidi kuboresha Afya Nchini.


Akizungumza katika kikao hicho Mkurugenzi wa Huduma za Afya Ustawi wa Jamii na Lishe Dkt. Ntuli Kapologwe amesema mradi wa USAID Boresha Afya umefanikisha kuboresha huduma za Afya Nchini ikiwemo ujenzi wa vituo bora vya Afya, upatikanaji wa vifaa na vifaa tiba, kuboresha na kuwezesha mazingira bora kwa watu wanaoishi na maambukizi ya VVU/UKIMWI kupata huduma katika vituo vyote vya Kutolea huduma za Afya Nchini.


Naye Mkurugenzi Mkaazi wa Shirika la Kimataifa la Watu wa Marekani (USAID Tanzania) Kate Somvongsiri amesema mpaka mradi huu kwisha wametumishi Dola za Kimarekani Mil. 220 sawa na fedha za Kitanzania Takribani sh bil 450 katika utekelezaji wa kazi mbalimbali za mradi huo.


USAID  imeweza kutoa ufadhili wa utekelezaji wa miradi miwili ambayo ni USAID boresha Afya mmoja ukiongozwa na EGPAF na mwingine ukitekelezwa na Deloitte kwa kuahirikiana na waahirika wenza EngenderHealth, MDH na FHI360.

No comments:

Post a Comment