Na Angela Msimbira Mwanga


Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.

 Ummy Mwalimu amesema kuwa ameridhishwa na ujenzi wa madarasa  katika Mkoa wa Kilimanjaro na kuamini kuwa utakuwa Mkoa wa kwanza kukamilisha ujenzi huo kwa wakati


Waziri Ummy ametoa pongezi hizo leo wakati alipokuwa kwenye ziara ya siku mbili mkoani hapo kwa lengo la kukagua Miradi ya Maendeleo inayotekelezwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Hai na Mwanga , Mkoani humo.


Amesema kuwa Mkoa wa Kilimanjaro utakuwa wa kwanza kukamilisha ujenzi wa madarasa  276 kati ya madarasa elfu 12 yanayotegemewa  kujengwa nchi nzima kupitia fedha za UVIKO 19 kwa lengo la kupunguza uhaba wa madarasa nchi nzima

amesema kuwa tarehe 24/11/2021 atatoa taarifa kwa umma kuhusu uchaguzi wa wanafunzi watakaojiunga na kidato cha kwanza kwa mwaka 2022, hivyo ukamilishaji wa madarasa  kutasaidia kuwawezesha watoto wengi kujiunga na kidato cha kwanza kwa wakati na hakutakuwa na watoto ambao watakosa nafasi ya kuendelea na masomo kwa sababu ya ukosefu wa madarasa nchini.


"Nimetembelea miradi ya ujenzi wa madarasa katika Mkoa wa Kilimanjaro  nimeridhishwa  na usimamizi unaofanyika kwa kuwa miradi iliyotekelezwa imeendana na thamani ya fedha zilizotolewa na Serikali, hivyo ni imani yangu kuwa miradi hiyo itakamilika kwa wakati uliopangwa” amesema Waziri Ummy


Aidha, Waziri Ummy amekamilisha ziara yake Mkoani Kilimanjaro ambapo alitembelea miradi ya Elimu, Afya na miradi ya ujenzi wa miundombinu ya barabara katika Halmashauri ya Wilaya ya Hai na Mwanga Mkoani Kilimanjaro.

Share To:

Post A Comment: