MKUU wa mkoa wa Tanga Adam Malima akisisitiza jambo kulia ni Kaimu Meneja wa Bandari ya Tanga Donald Ngaire  na aliyesimama nyuma ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga (RAS) Pili
KAIMU Meneja wa Bandari ya Tanga Donald Ngaire akizungumza
MKUU wa Mkoa wa Tanga Adam Malima  katika akitembelea Bandari ya Tanga mara baada ya kukabidhi vifaa kulia ni Kaimu Meneja wa Bandari ya Tanga Donald Ngaire

BANDARI ya Tanga itakuwa na uwezo wa kuhudumia tani Milioni 3,000,000 kwa mwaka kutoka Tani 750,000 za awali kwa mwaka baada ya kukamilika kwa ujenzi wa Gati Mpya ambapo ujenzi wake kwa sasa unaendelea.

Hayo yalisemwa  na Kaimu Meneja wa Bandari ya Tanga Donald Ngaire wakati wa halfa ya kupokea vifaa vya kuimarisha utendaji na ufanisi kwenye Bandari hiyo kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga Adam Malima vifaa vilivyotolewa ni mashine ya Crane 3 pamoja na Pilot Boti 1 Mpya.

Ambapo alisema shehena hiyo itaongezeka matarajio ya mamlaka  kuongeza mapato yanayotokana na huduma zitakazokuwa zikifanyika kwenye Bandari hiyo sambamba na uongezaji wa vifaa vitakavyoongeza ufanisi ambao utakuwa na tija kubwa.

Alisema pia vifaa hivyo vitasaidia kuimarisha utendaji kazi  na hata muda wa meli kukaa bandarini utapungua ikiwemo kuvutia biashara kutokana kwa wafanyabiashara ambao wanaitumia Bandari hiyo kupitisha shehena zao za bidhaa mbalimbali .

“Kikubwa ni kwamba uwepo wa vifaa hivi  utavutia biashara kwani anapokuja mteja kukuta vifaa vichache vitamvunja moyo hivyo uwepo wake itachochea watu wengi kupitisha mizigo yao hapo sambamba na kuimarisha utendaji na ufanisi”Alisema

Awali akizungumza Mkuu wa Mkoa wa Tanga Adam Malima alisema kwamba Serikali ya awamu ya Sita imekusudia kuifanya Tanga kuwa kitovu cha kusafarisha mizigo nje ya nchi na ndani ya Tanzania ipo pale pale na amekuwa akihimiza kila wakati.

Alisema kuwa Rais Samia ameliweka hilo na amekuwa akihimiza kila wakati kutokana na kutaka kujua maendeleo yake na akija yeye au makamu wa Rais au wakija viongozi wa kitaifa watawapeleka kwenye Bandari hiyo ili waweze kuona mafanikio makubwa ya  uwezekaji uliofanyika  kwa ajili ya manufaa ya watanzania wote.

“Tunamshukuru Mh Rais ameliweka hilo na amekuwa akituhimiza na hata wakati mwengine kupiga simu kujua maendeleo yake akija yeye au makamu wa Rais au viongozi wengine wa kitaifa tutawaleta hapa kwenye Bandari kuona mafanikio makubwa ya uwekezaji uliofanyika kwa ajili ya manufaa ya Watanzania wote”Alisema

Alisema mita mia za kwanza hii novemba wamebakiwa miezi mitatu wakabidhiwa mita hivo mia na meli ziweze kuegesga hapo hapo Bandarini na ni matarajio yake wakati yanafanyika hayo wapo kwenye mchakatoo wa uwekezaji Treni kuingia bandarini ili kuchukua mizigo hapo kupeleka Bandari ya Bandari Kavu Arusha.

Alisema ile fikra ya kwamba ikija meli huku akieleza kwamba Novemba 20 mwaka huu inaingia meli ya Clinka tani elfu 50 itapakua mzigo na kula nje meli ya mafuta itaingia tani 49000 ukiachilia mizigo midogo na huo bado uwekezaji haujakamilika wanapokuwa nje wakija hapo mambo yatakuwa makubwa na itakuwa ndogo hivyo wameshauri mwishoni mwa mwezi watakutane na viongozi wa reli nchini,Bandari na Serikali ya Mkoa wa Arusha.

Mkuu huyo wa mkoa alisema  watakaa kwa pamoja wajadiliane na wizara ya ujenzi  wafanye uwekezaji huo mkubwa wa mabilioni hapa Tanga halafu watakuwa wamefinywa na wanahitaji nafasi ya kupumulia na nafasi hiyo ni Bandari kavu ya Bandari ya Tanga iliyopo eneo la Marula Arusha yenye ekari 200.

Aliongeza kwamba  wakati wanatengeneza hiyo wataishauri serikali uwekezaji huo uendane na nafasi ya kupumlia mizigo huko kutokana na kwamba ukitoka Tanga hadi Arusha unakutana na magari  zaidi ya 50 kila siku wanakuja kupakua mizigo yao na ni mzigo mikubwa hakuna sababu wakati reli ipo watakuwa wanakuja na wakifika Marula watachukua mizigo yao.

Mwisho.


Share To:

TANGA RAHA BLOG

Post A Comment: