Tuesday, 30 November 2021

KENNANI KIHONGOSI ALIVYOZINDUA KAMPENI NGORONGORO

Katibu Mkuu wa Umoja wa  Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Kennani Kihongosi amezindua kampeni za Ubunge Jimbo la Ngorongoro Mkoani Arusha

Kihongosi amesema mgombea huyo Emanuel Shangai, anatosha kurithi viatu vya aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo ambaye pia alikuwa Naibu Waziri wa Uwekezaji William Tate Ole Nasha.

Uzinduzi wa kampeni hizo katika Tarafa ya Ngorongoro umefanyika katika viwanja vya kata ya Ngoile, ambapo Chama cha Mapinduzi  kimetumia fursa hiyo kumsimamisha Ndugu Emmanuel Shangai na kumkabidhi Ilani ya Uchaguzi ya 2020/2025 ya Chama hicho.

Katika hatua hiyo, Kihongosi alisisitiza kuwa Shangai ana uzoefu wa uongozi katika kutetea maslahi ya wananchi wa Ushetu, hususani katika masuala ya elimu, afya na maboresho ya miundombinu kwani mgombea huyo amekuwa diwani na Mwenyekiti wa Halmashauri hivyo atakuwa mtetezi wa wananchi wa Ngorongoro.

Katibu Mkuu huyo wa UVCCM ataendelea kuzunguka katika maeneo mbalimbali ya Jimbo la Ngorongoro ili kuweza kuzungumza na wananchi wa Jimbo hilo  na kuwaelesha kwa usahihi wa hoja juu ya mafanikio ya Serikali ya Chama cha Mapinduzi na Mipango kazi, Sera na Mikakati iliyopo kwenye Ilani ya CCM ambayo Emmnauel Shangai atakapochaguliwa kuwa mbunge wa jimbo hilo ataenda kuitekeleza.No comments:

Post a Comment