Sunday, 7 November 2021

KAMATI ZA BUNGE ZATAKIWA KUCHUKUA HATUA KATIKA SHERIA ZA USAWA WA JINSIA Na Mwandishi Wetu - Dodoma

Kituo cha haki za binadamu  (LHRC) imesisitiza kuhusu mapendekezo  ya Sheria zilizopitishwa ambazo hazijachukuliwa  na kamati tathimini hiyo imeona kwamba mapendekezo yanayohusiana uzingatiaji wa usawa wa kijinsia Kama vile usawa kati ya wanawake na wanaume katika bodi  au kamati zinazoanzishwa kisheria  na mahitaji ya makundi  Maalumu hayajachukuliwa.

Hayo yamezungumzwa leo na  Mratibu wa mtandao wa wanawake  watetezi wa haki za binadamu Tanzania  Hilda Dadu wakati akiwasilisha ripoti ya matokeo ya uchambuzi wa mapendekezo ya miswada kuwa Sheria kwa kamati ya Bunge ya sheria iliyofanyika Leo jijini Dodoma.

Aidha Dadu amesema kuwa mapendekezo yaliyolenga kuishauri kamati kupunguza adhabu  na kuondoa adhabu za jumla katika Sheria nayo hayakuchukuliwa 

" Tunaomba na kusikitisha kamati kuangalia upya suala law adhabu za jumla pamoja na viwango vikubwa vya adhabu hizo, tunatoa wito mbele ya kamati hii kuwa utunzi wa sheria  uepuke adhabu za jumla hii itawezekana endapo adhabu itokane na kifungu husika cha sheria kilichokiukwa kulingana na uzito wake" - Dadu.

Hata hivyo Dadu alimaliza kwa kusema kituo hicho kinaendelea kutuma maombi kwa kamatie na kuyapa jichoe la kipekeee na msisitizo kwa mapendekezo hayo kwa wakati ujao.

No comments:

Post a Comment