Na. Angela Msimbira Kilimanjaro


Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe Ummy Mwalimu ameziagiza Halmashauri zote Nchini kuhakikisha zinakamilisha ujenzi wa Madarasa  ifikapo tarehe 15.12.2021


Akikagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Halmashauri ya Wilaya ya Hai Mkoani Kilimanjaro Mhe. Ummy amesema hakutakuwa na uchaguzi wa awamu pili  ya wanafunzi wa kidato cha kwanza  hivyo ameziagiza Halmashauri zote kuhakikisha wanakamilisha  ujenzi wa madarasa kwa wakati ili wanafunzi wote wanaofaulu kujiunga na kidato cha kwanza wanaanza  kusoma kwa wakati mmoja.


Amesema fedha za UVIKO 19 zimetolewa kwa lengo la  kuendeleza miradi ya maendeleo kwenye  sekta ya afya, na elimu hivyo Viongozi wa Mikoa yote nchini  wanawajibu  wa  kuhakikisha wanasimamia kikamilifu ukamilishaji wa ujenzi wa   miradi kwa wakati.


Waziri Ummy ametoa maelekezo juu ya kutumia mapaa yenye migongo miwili ili kupunguza gharama za ujenzi na kuhusu matumizi ya vigae amewataka kutumia tarazo au sakafu za kawaida kwa kuwa vigae vinavyowekwa kwenye ujenzi wa madarasa vipo chini ya viwango.


Aidha kwa Halmashauri ya Wilaya ya Hai imepata kiasi cha shilingi milioni   860 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa 42

Share To:

Post A Comment: