Na Rhoda Simba Dodoma


WARATIBU wa Sensa ya majaribio wa Mikoa na Wilaya na wasaidizi  wao wamekutana jijini Dodoma na kutoa mrejesho juu ya Sensa ya majaribio iliyofanyika mwezi Septemba mwaka huu ili kujadili chanagomoto zilizojitokeza na kuzifanyia kazi kabla ya kufikia sensa ya watu na makazi mwaka 2022.


Akiongea leo katika mkutano wa  Tathmini ya Sensa ya majaribio iliyofanyika mapema mwezi wa 9 mwaka huu Kamisaa wa Sensa ya Watu na Makazi Anna Makinda amesema majaribio hayo  yanatokana na maandalizi ya sensa ya mwaka katika nchi kutokana na kanununa na Taratibu za Umoja wa Mataifa sensa hufanyika kila baada ya kumalizika kwa sensa moja ambapo wataalamu wanatakiwa kuanza maandalizi ya sensa ya mwaka mwengine.


" Sisi hapa Tanzania baada ya kumalizika kwa Sensa mwaka 2012 wataalamu wetu walikaa na kuona ni namna gani Sensa ya mwaka 2022 itakavyokuwa," amesema Makinda.


Na kuendelea kusema kuwa  "Kabla ya mwaka mmoja waliteuwa Mikoa 18 ya majaribio kijiji na vitongoji kadhaa lengo likiwa nikutaka kuona Sensa ya mwaka 2022 yako vizuri au kuna vitu vinatakiwa kuongezwa," Amesema .


Amesema Vingozi hao wamekutana na kuleta mrejesho kama Sensa ya majaribio ilikuwa na changamoto gani kitu gani kiongezwe na kuponguza kwenye  madodoso hata kwenye matumizi ya vishikwambi kama vilikuwa na matatizo au vilikuwa sawa ambapo mpaka  mwisho wa mwezi huu zoezi hili litakuwa limekwisha.


Tukumbuke Rais Samia Suluhu Hassan alizindua mkakati  wa elimu na uhamasishaji wa Sensa 2022 lengo alitutaka sisi wasaidizi wake twende kuwaelimisha wananchi ili ifikapo siku hiyo kila mtua aweze kuandikishwa na kihesabiwa sehemu yoyote ulipo utafikiwa na kuhesabiwa. 


Mwishoo

Share To:

Post A Comment: