Jane Edward, ArushaWananchi wametakiwa kuzitumia huduma za posta ambazo zimeboreshwa kidigitali kupitia Tehama .


Hayo yamesemwa na Kaimu postamasta Mkuu  shirika la posta Tanzania,Macrice Mbodo wakati akizungumza katika mkutano wa wadau wa Tehama unaofanyika mjini hapa.


Amesema kuwa,Serikali ya awamu ya sita chini ya Mh Samia suluhu Hassan imejipanga kutumia Tehema kurahisisha utoaji wa  huduma za  serikali  kwa wananchi kupitia vituo  vya huduma pamoja.


Amesema ,Serikali imejipanga kupitia shirika la posta  Tanzania kuhakikisha kuwa huduma mbalimbali za serikali zinatolewa chini ya dari Moja kupitia vituo vya huduma pamoja.


Mbodo amesema kuwa, wameshiriki mkutano huo  ili kuonyesha fursa ya kidigitali inayotumiwa na   posta kwani posta  waliyonayo kwa sasa sio ile ya zamani.Ameongeza kuwa ,posta ya kidigitali inamwezesha mwananchi kuwa na duka mtandao ambapo inamwezesha  mwananchi kuuza na kununua bidhaa zao kote duniani  kupitia duka hilo .Kwa upande wake inspekta Reuben Komba meneja tehama shirika la posta  Tanzania amesema shirika limepiga hatua kubwa hasa katika kushughulikia mambo ya tehama kidigitali.


"Shirika hili la posta Tanzania kwa sasa limekuja na mkakati kabambe wa kuhakikisha kuwa pamoja na mambo mengine linajikita katika kuziweka huduma za posta kiganjani ili iwe rahisi huduma zake kupatikana"Alisema


Ameongeza kuwa mpango mkakati wa kitengo cha tehama ni kuhakikisha wananchi wa vijijini na mijini wanafikika kwa urahisi kidigitali.


Amewataka wananchi kuwa wazalendo na kuviunga mkono vitu vinavyoanzishwa hapa nyumbani na sio kukimbilia vitu vya nje.


Mwisho,......

Share To:

Post A Comment: